Wednesday, 19 June 2013

Tundu Lissu na wenzake kufikishwa Mahakamani



 Haya ni makasha ya mabomu yaliyorushwa na Askari wa Jeshi la Polisi jana kwa nia ya kuwatawanya wafuasi wa Chadema katika Uwanja wa Soweto.Picha kwa hisani ya Jamiiblogu.


WAKATI Wabunge wanne wa Chadema, Said Arfi (Mpanda Mjini), Tundu Lissu (Singida Mashariki), Mustapha Akunaay (Mbulu) na Joyce Mukya (Viti Maalumu), wakifikishwa katika Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Arusha Asubuhi hii kujibu mashitaka yao, hali katika jiji la Arusha haijawa shwari kwani wafuasi wa chama hicho wameanza kukusanyika tena katika Uwanja wa Soweto kwa ajili ya maombolezo.
Mbali na Uwanjani hapo, kundi la vijana mbalimbali pia wametinga katika Kituo Kikuu cha Polisi Mkaoni hapa, kwa ajili ya kushudia msafara wa wabunge wa waliokamatwa jana kwenda Mahakamani.
Akizungumza na Waandishi wa Habari dakika chache zilizopita Mkuu wa Operesheni wa Polisi, Kamishna Paul Chagonja amesema kwamba, Jeshi la Polisi litaendelea kulinda amani jijini hapa na kuwataka wananchi wasiendelea kukaa katika mikusanyiko isiyo halali, badala yake waendelee na shuguli zao na kujitafutia ziriki.
Hata hivyo Chagonja alisema kwamba Jeshi hilo pia linamtaka Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe na Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema, wajisalimishe wenyewe kabla ya nguvu ya kuwakamata hazijatumika rasmi.
"Minapenda kuwaomba wananchi wa Jiji la Arusha, waendelee na kazi za kujitafutia riziki waachane na suala la kukaa kwenye vikundi na mikutano isiyokuwa kibali cha Jeshi la Polisi,lakini pia naomba kutumia nafasi hii kumtaka Mbowe na Lema wajisalimishe wenye kwa Jeshi la Polisi popote walipo kabla hatujatumia nguvu kuwasaka na kuwakamata"alisema Kamishna Chagonja.

No comments:

Post a Comment