Monday, 10 June 2013

Wenye tabia hizi kuanzia sasa hawatakiwi Facebook



HATIMAYE mtandao wa Facebook umeamua kuja na teknolojia mpya ya kuwathibiti, watumiaji wa mtandao huo kwa njia zisozo sahihi ikiwa ni pamoja na kuweka picha za ngono.
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta ndiye aliyekuwa mtu wa kwanza kuingia katika teknolojia hiyo baada ya kuingia katika mfumo huo wa verified Account, Rais Kenyatta aliweza kuingia katika hatua hiyo kupitia kundi la watu maarufu duniani na wenye wafuasi wengi katika mtandao huo.
Hatua hiyo itakuwa sawa na mtandao wa Twitter kwa kuanzisha akaunti na kurasa zilizothibitishwa (verified pages/accounts) ili kuwawezesha watu maarufu kuthibitisha akaunti zao pamoja na akaunti na mashabiki wao katika kurasa zao.
Katika taarifa yake mtandao huo ulifafanua kwamba teknolojia hiyo itawasaidia watumiaji wa Facebook kuzitambua akaunti za kweli za watu maarufu  wanaotumia mtandao huo, pamoja na kutambua watu wanaotumia account feki kwa ajili ya kuchafua majina ya watu wengine hususan majina ya watu maarufu katika jamii.

No comments:

Post a Comment