
NINA
furaha sana moyoni. Hii ni kwa sababu ninakwenda kukupa kitu kizuri
sana ambacho kitakusaidia katika maisha yako ya uhusiano. Kwa hakika
hutajutia muda wako kusoma ukurasa huu.
Marafiki
zangu, ukisoma kichwa cha habari kwa haraka, unaweza kuona kama mada ni
ya kawaida sana, ambayo imezoeleka katika jamii yetu. Let me tell you
something; it’s not as simple as many people think. There is a big thing
which you are going to learn.
Kuchokana
ni tatizo kubwa tena linalogharimu uhusiano wa wengi. Wanashindwa
kufanya mambo mengine ya msingi kwa sababu ndani ya nyumba hakuna
furaha. Hakuna maelewano. Kama yapo ni ya kuigiza tu.
Kwa
nini yote hayo? Wamechokana. Kitu kikubwa kwako ni kutuliza ubongo wako
sawasawa kuweza kupokea kitu cha kipekee na cha tofauti kabisa. Je,
unahisi kumchoka mpenzi wako? Unadhani mwenzi wako amekuchoka? Leo
unakwenda kupata ufumbuzi.
KUCHOKANA NI NINI HASA?
Unaweza
kutafsiri vyovyote uwezavyo. Kila mmoja anaweza kuwa na maana yake kwa
mtazamo wake, lakini mwisho maana huwa ni moja tu, kuchokana! Kimsingi
ni neno linalotokana na kuchoka.
Wengi
wanafahamu vyema maana ya uchovu. Hapa kwenye All About Love, tafsiri
moja rahisi ni kumuona mwenzako wa kawaida. Kumzoea kupita kiasi na
kuhisi wa kawaida tu (kumshusha thamani).
Ukimchoka
mpenzi wako ni vigumu hata kuhisi kukutana naye faragha. Wa nini?
Unamchukulia wa kawaida tu, kama sehemu ya maisha yako, lakini si muhimu
wala wa kipekee kama ilivyokuwa mwanzo. Umenipata ninachozungumzia?
Tuendelee kujifunza.
NI KWELI WAPENZI HUCHOKANA?
Wapo
wasioamini kama kuna suala la wapenzi kuchokana. Kama wewe ni mmoja
wapo, unawaza tofauti sana rafiki yangu. Kuchokana kupo kwenye mapenzi.
Kuna sababu kadha wa kadha zinazosababisha hali hiyo, lakini nyingi ni
zile za kujisahau zaidi!
Tatizo
hili huwaathiri zaidi wanandoa (hasa waliopata watoto), wale ambao
hawana, tatizo huanza kujitokeza katika umri wa ndoa wa kuanzia miaka
miwili na kuendelea.
Kwa
mapenzi ya siku hizi, hata miezi sita tu ya mwanzo wa ndoa, wenzi
huanza kuchokana kwa sababu mbalimbali. Unajua kinachotokea baada ya
wenzi kuchokana? Darasa linaendelea...
HALAFU...?
Matokeo
ya yote hayo hapo juu si mazuri. Ni usaliti. Ukimchoka mume/mke wako,
maana yake huwezi kuwa naye, utajilazimisha inapobidi. Kama mwanaume
akimchoka mkewe ni hatari zaidi, maana anaweza kukaa kimya bila kutaka
kukutana naye, wakati yeye akiendelea na mambo yake huko nje.
Mwanamke
kwa sababu ameumbwa na woga, si mwepesi kuwa wa kwanza kutaka faragha
na hapa ndiyo chanzo cha yeye kusaka pumziko nje ya ndoa yake. Mwanaume
anasaliti na mke naye anasaliti. Unaona matatizo hayo?
Mazoea
ninayoyazungumza hapa huzorotesha ubora wa tendo la ndoa. Kwa kuwa
mnaonana wa kawaida, hata faragha yenu haiwezi kuwa ya mahaba. Kwa
mtindo huo ni dhahiri kwamba, kila mmoja atakuwa anabaki na kiu yake na
huenda akafikiria kutafuta mahali pa kuikata!
Habari
mbaya zaidi ni kwa wanawake ambao wengi hubaki na maumivu kwa muda
mrefu. Nimeshakutana na kesi za namna hiyo mara nyingi sana. Ngoja
nitakupa mifano mitatu tu ya haraka.
WASIKIE HAWA...
Msomaji wa kwanza:
Kaka
Shaluwa mimi nina mpenzi wangu, nimedumu naye kwa miaka mitatu sasa.
Tatizo kubwa ni kwamba mwenzangu hajawahi kumaliza haja zangu hata siku
moja.
Kila siku amekuwa akifurahia peke yake na kuniacha kama nilivyokuwa mwanzoni. Tatizo ni nini? Naomba msaada wako.
Msomaji wa pili:
Hi
kaka Shaluwa. Mimi ni msichana mwenye umri wa miaka 24, nina mpenzi
wangu, mtu mzima kidogo. Tuna miaka miwili tangu tumeoana. Tumebahatika
mtoto mmoja wa kiume. Tatizo ni kwamba sijawahi kufurahia tendo hata
mara moja.
Nimeshawaza
kutoka nje, lakini naogopa maana nampenda sana na ninaogopa akijua
anaweza kuniacha. Tafadhali kaka, nisaidie kuokoa ndoa yangu.
Msomaji wa tatu:
Habari.
Mimi ni mama nina umri wa miaka 34, nina watoto wanne, naishi Tabora na
mume wangu. Nina tatizo katika ndoa yangu. Mume wangu hanipi starehe
faragha. Huwa ananirukia mara moja tayari...ananiacha nipo vile vile.
Nini
tatizo kaka yangu? Naomba unisaidie tatizo hili tafadhali. Sitaki
kutoka nje ya ndoa yangu, bado nampenda sana mume wangu. Nifanyeje?
No comments:
Post a Comment