Kiongozi wa Kanisa Katoliki ulimwenguni Papa Francis amesema
hawezi kuwahukumu mashoga, lakini akalaani kampeni ya
kuhalalisha ushoga akiiita tatizo kubwa. Vile vile Papa Francis
amesema kanisa halina budi kuwapa wanawake majukumu
makubwa, ingawa amesema kuwa milango ya wao kuwa mapadre
imefungwa.
Akizungumza na waandishi wa habari kwenye ndege yake akitokea
Brazil kurudi Roma, Papa Francis alisema kuwa shoga sio tatizo,
tatizo kampeni ya kuuhalilisha. Alisema kama mtu ni shoga na
anamtafuta mungu kwa nia ya dhati, basi yeye hawezi kumhuku.
Kiongozi huyo wa wakatoliki ulimwenguni alijibu maswali kuhusu
mtu aliyemteuwa kuongoza banki ya Vatican yenye matatizo,
Battista Ricca, ambaye licha ya uteuzi huo anasakamwa na shutuma
ya kuwa na uhusiano wa kingono na shoga. Papa amesema aliagiza
uchunguzi mfupi juu ya madai hayo, lakini hakukua na ushahidi
wowote dhidi ya mtu huyo.
No comments:
Post a Comment