Wednesday 25 September 2013

FAHAMU HASARA ZA MAPENZI KATIKA UJANA.

Ni kweli watu hukasirika iwapo mmoja anavunja mahusiano kati yao, hata kama ngono haikuhusika.
Lakini hali ya kujisikia kusalitiwa inakuwa kubwa zaidi iwapo ngono imekuwa sehemu ya uhusiano huo.
Ngono inaweza kuwasha mlipuko wa mihemuko na kumfanya mtu afikiri kuwa uhusiano kweli ni wa uhakika, kwamba kila mmoja anampenda mwenzake.
Inaweza kujenga uhusiano mkubwa wa kimhemuko na kuumiza sana unapovunjika, hasa ikigundulika kuwa mmoja kati yao hakuwa na mapenzi yenye kuwajibika.
Kwani hali ya kujisikia kusalitiwa inaweza kuzaa hasira, na hata vurugu.
Katika kitabu cha ‘Sex and Teenager,’ Kieran Sawyer anaandika hivi: “Kwa kadiri uhusiano unavyoonekana kuwa na upendo halisi, ndivyo hivyo kijana anavyowekeza kujenga mapenzi ya kudumu.
Na ndivyo hivyo yanavyokuwa maumivu makali kama mapenzi hayo yatavunjika,” Wakati mwingine kuvunjika kwa mapenzi kunatokana na kufuatiwa na ghadhabu kali.
Ghadhabu hii ni hasira inayoweza kuwafanya vijana wengine kujiua.
Katika miaka 25 iliyopita idadi ya vijana waliojiua kwa sababu ya kuvunjika kwa mahusiano ya kimapenzi iliongezeka mara tatu.
Utafiti uliofanyika mwaka 1988 na Idara ya Health and Human Services ya Marekani umeonyesha kuwa msichana mmoja kati ya watano amejaribu kujiua wakati kwa wavulana mmoja kati ya kumi alifanya hivyo.
Hiki ni kipindi ambacho kiwango cha vijana waliojiingiza katika vitendo vya mapenzi kiliongezeka kwa ghafla, hasa kwa wasichana.
Hakuna shaka kuwa vitendo vya kujiua vinatokana na matatizo mengi, lakini tukizingatia yale tuyajuayo kuhusu hasira zitokanazo na kuvunjika kwa mapenzi ni halali kufikiri kuwa maumivu yatokanayo na kuvunjika huko ni sababu ya kutosha kuthibitisha viwango vya kujinyonga kunakofanywa na vijana wengi.
Ngono inaweza kuwa na madhara mengine ya kivionjo inayoweza kubadilisha mahusiano mazuri kuwa mabaya.
Katika hali hiyo maeneo mengine yanayoguswa na mahusiano hayo hudumishwa. Punde kidogo mahusiano hasi huanza kujitokeza.
Hatimaye kuweka sumu katika mahusiano hayo na kile kilichokuwa kitamu hugeuka kuwa kichungu.
Mwanamke mmoja anatueleza kisa kinachoeleza hali hiyo: “Kwa kadiri tulivyowekeana ahadi ya kukutana, maombi ya ngono kutoka kwa mpenzi wangu yakawa yananiaminisha zaidi.
‘‘Kwa kweli tulipendana sana. Katika miezi miwili nilisalimu amri, kwa vile nilikuwa sasa na hakika ya mahusiano yetu. Katika miezi sita mingine ngono ikawa kiini cha mahusiano yetu.
“Wakati huo huo, mambo mengine mapya yakaingia katika uhusiano wetu kama hasira, kukosa uvumilivu, wivu na ubinafsi. Tukakoma kabisa kuongea, kwa hiyo tukajiona tunachukizana. Nikatamani nipate mabadiliko,” anasema.
Msichana mmoja (22) anasema akiwa bado bikira alitoa onyo hili kuhusu kujihusisha kimapenzi katika umri mdogo: “Nimewaona marafiki zangu wengi ambao kuvujika kwa mahusiano yao kuligeuka kuwa mapambano ya kimwili.
‘‘Uharibifu wa vionjo vya mapenzi unatisha, kwa vile wamekuwa wameshirikiana kitu fulani chenye nguvu sana maishani mwao. Unapotumia ngono katika umri mdogo, utazuia mawasiliano mengine ya kimapenzi na yaweza kudumaza kukua kwa mahusiano mengine,” anasema.
Kujihusisha katika mapenzi mapema siyo tu kunadumaza makuzi ya kimahusiano, bali pia kunadumaza kukua kibinafsi.
Baadhi ya vijana wanadhani kujiingiza katika matumizi ya dawa za kulevya na pombe kutawaondolea matatizo yao, wengine wanafikiri wataondoa ghadhabu zao kwa kufanya vitendo vya ngono.
Ngono inakuwa kisingizio. Hawajifunzi kukabiliana na matatizo ya maisha.
Vijana waliojiingiza katika mahusiano ya kimahaba wanajifunika ndani katika kipindi ambapo walitakiwa wajifunue na kuunda mahusiano mapya, kujishughulisha na vilabu mbalimbali vya burudani, wakiendeleza ujuzi na stadi za maisha na kuchukua nafasi kubwa katika majukumu ya kijamii.
Yote hayo ni virutubisho vizuri katika makuzi ya binadamu.
Kipindi hiki cha maisha ni cha pekee kwa vijana kwa vile wana muda na nafasi ya kuendeleza vipaji na mapendeleo yao.
Kukua kunakotokea sasa katika maisha yao kutaathiri maisha yao yote. Kama nyie vijana hamtumii miaka ya ujana vizuri, hamtaweza kukua katika ukamilifu upasao.
Hatari inakuwa kubwa zaidi kwa wasichana wanaojihusisha kimapenzi na kwa kufanya hivyo wanafunga milango katika mahusiano mengine.
Mtaalamu Samuel Kaufman wa New York anasema: “Msichana anayejiingiza katika mahusiano ya kimapenzi na mvulana katika umri wake mdogo, baadaye anawaza utu wake uliharibiwa.
‘‘Alikuwa sehemu ya huyo mvulana na akashindwa kuendeleza matashi yake na kuharibu hali yake ya upekee.”
Akitafakari uzoefu wake wa muda mrefu katika ushauri nasaha wa vijana wa chuo kuhusu masuala ya jinsia, Dk. Carson Daly anatoa mawazo akisema: “Sifikirii kuwa nimewahi kumkuta mwanafunzi aliyejutia kuahirisha tendo la ngono, lakini kwa hakika nimekutana na wengine waliojutia baada ya kujihusisha na mapenzi.
‘‘ Tena na tena nimeona madhara ya muda mrefu ya vionjo na kutengwa kiroho kunakotokana na ngono holela na uasherati. Hakuna anayesema kuwa wakati mwingine inachukua muda mrefu kupona kutokana na majeraha ya mahusiano ya kingono, wengine hawaponi kabisa.”
Mapenzi yaweza kuwa chanzo cha starehe au furaha, lakini ieleweke wazi vijana wanahitaji msaada na maelekezo ya watu wazima ili waelewe masuala hayo vizuri.
Ngono inaweza kuwa chanzo cha majereha makubwa na mateso. Kinacholeta tofauti ni mahusiano yanayotokea. Ngono huleta furaha na ukamilisho salama kivionjo na kimwili, ikifanyika katika mahusiano ya kimapenzi yenye upendo wa kweli, uliotimilifu na wenye kuwajibika.
Kihistoria tumeiita ngono katika mahusiano ya namna hiyo. Umoja wa kingono ni sehemu ya jambo lililokubwa la ushirika wa maisha ya nafsi mbili

No comments:

Post a Comment