KAMA
ilivyo ada tumekutana tena ili kujuzana machache kuhusiana na maisha
yetu ya kila siku. Nina imani kichwa cha makala kitakushtua, hasa
wanawake. Siku zote kona hii imekuwa ikifanya uchunguzi wa kina na
majibu yake huwa hayana shaka kwa jamii.
Kona
hii imekuwa ikisisitiza umuhimu wa ukweli na uwazi katika mapenzi
ambapo huwafanya wapenzi waondoe wasiwasi kwa wenza wao kutokana na
kuwajua kiundani.
Kwa nini wanapenda kudanganywa?
Siku
zote kiumbe wa kike hupenda vitu vizuri, kwa mfano kumpata bwana mzuri
mwenye fedha na uwezo wa kitandani, hakuna mwanamke anayependa kinyume
na hayo niliyoyataja, yakikosekana ataendelea kutafuta mtu sahihi
atakayekubalika moyoni mwake.
Tupo
pamoja? Najua unaweza ukajiuliza mbona wewe haupo hivyo na hata mpenzi
wako hana kipato, pia hata maneno yake yamejaa maudhi lakini bado upo
naye!
Siku
zote utafiti wa jambo fulani unaweza ukafanywa na watu 10. Kama kuna
wanawake 10, sita kati yao wakapenda kufanya kitu fulani wakati wengine
wanne nao wakaegemea upande wa pili, wale sita ndiyo watatoa jibu la
wanawake wengi wanapenda nini.
Katika uchunguzi wangu pamoja kuwasoma wanawake wengi ninapozungumza nao, nimegundua vitu hivi:
Vitu gani?
Kama
nilivyosema awali mwanamke ni kiumbe kilichoumbwa kwa ajili ya kupamba
dunia, hivyo kinapenda raha, shida ikitokea huwa bahati mbaya, sawa na
kumfunga mbuzi mnyororo.
Tumeshuhudia wanaume wengi wa ukweli wakikimbiwa na wanawake baada tu ya kuonekana hawana vigezo, hasa uwezo wa kimaisha.
Pia
tumeshuhudia wanawake wakiingizwa mkenge kutokana na kukutana na
wanaume matapeli wa mapenzi kwa kujikweza wana fedha au nyadhifa kubwa
serikalini. Hapo mwanamke huingia kichwakichwa na kuachwa solemba baada
ya mhusika kukidhi haja zake za kimwili.
Tabia hii imewafundisha nini wanaume?
Tabia
ya baadhi ya wanawake ambao ni asilimia kubwa, kupenda vitu vizuri,
imesababisha kila mwanaume kutengeneza uongo ili ampate mwanamke fulani.
Wapo
wanaoazima nguo, magari na hata vyumba, kwa kuhofia akienda alivyo,
hawezi kukubaliwa. Kwa maana hiyo narudi tena kwenye kichwa cha habari
kuwa wanawake wanapenda kudanganywa kuliko kuambiwa ukweli.
Madhara
yake nini?
Kutokana
na watu wengi kuishi maisha ya maigizo ili wampate msichana, wasichana
wengi huharibiwa ndoto zao za kuishi maisha mazuri na kuwa ‘vishata’.
Wengi
wakishaujua ukweli kuwa mwanaume aliyenaye ni kula kulala, hana kazi,
analala chumba cha watu watano, chumba alichotumia wakati wa kukutongoza
ni cha rafiki yake, gari alilokuwa akitumia kukufuata pia la rafiki
yake, husitisha mapenzi.
Inawezekana
kabisa matangazo ya mwanaume mwongo yalisababisha hata kuachana na
mpenzi wako mliyekuwa na malengo naye, wengine hufikia hatua ya kuvunja
ndoa zao.
Nini cha kufanya?
Ni
kweli kila kiumbe kinapenda maisha mazuri, lakini maisha hayo hayaji
kwa lazima bali kwa kujituma, kuvumilia na kuikubali hali yoyote, si
kutaka vizuri tu.
Penda ukweli na uwazi ili uingie kwenye penzi ukiwa unamjua kiundani mpenzi wako na kuamini ipo siku mtapata.
Usipende
kuishi maisha ya mtu mwingine, acha tamaa, kama shoga yako kapata,
subiri na wewe zamu yako, kwa vile Mungu si wa mmoja. Maskini naye ni
mtu, msikilize ili kuepuka kulazimisha kudanganywa.
No comments:
Post a Comment