Thursday, 19 September 2013
Ngono kabla ya ndoa ni tofauti na nje ya ndoa!
Nisingependa kuegemea sana kwenye maandiko ya dini mbili ninazo amini ili kuepuka kuigawa jamii ya wasomaji wangu, ila napenda kukumbusha tu kuwa kuna maandiko yenye maana sawa na “mjizuie/msioe lakini mkishindawa kutokana na tamaa/mahitaji ya mwili basi na muoe, mwili wa mwanamke sio wake pekee bali pia ni wa mume wake hali kadhalika wa mwili wa mwanaume sio wake pekee bali ni wa mkewe”.
Hivyo ukiangalia kwa undani hapo utagundua kuwa nia na madhumuni ya kuoa/olewa ni kungonoana alafu swala la kuzaliana ni matunda ya tendo hilo takatifu na mengine yanafuata(nitalizungumzia hili nkirudi).
Swala la kusubiri ngono mpaka ufunge ndoa linasisitizwa na dini mbili nizijuazo mimi lakini pia Miiko na Mila mbali mbali zina amini nakusisitiza hilo wakati baadhi yao ngono inafanywa mara tu kijana au binti anapobalehe/kua/Pevuka na ngono hiyo hufanywa kati ya binti/kijana na ndugu wa mwanzo wa familia kama vile baba/binamu/shangazi(wanakufungua kabla hujaenda kuolewa/oa).
Tunapozungumzia swala la kutokufanya ngono kabla ya ndoa kwa kufuata Miiko au Imani zetu basi ni vema kama tukawa tunafanya kila jambo linalotakiwa kwenye Miiko na Imani tunazoamini, lakini wangapi wanasubiri ngono mpaka ndoa na wanafanya kila lililojema linalosisitizwa kwenye vitabu vya imani zao?
Nakubali kuanzia miaka ile mimi nakua (90s) kumekuwa na mlipuko wa watu kufanya ngono kabla ya ndoa, hali iliyo sababishwa na inaendelea kusababishwa na mambo mbali mbali likiwemo swala zima la uchumi, kubaki shuleni kwa muda mrefu, kugundulika kwa utamu wa ngono kwa wanawake wengi kwamba ngono sasa sio chanzo cha kuzaliana tu bali ni sehemu ya kufurahia ujinsia wetu tofauti na zamani ambapo lengo na madhumuni la tendo hili lilikuwa ni kumpa raha mume na kuendeleza vizazi.
Kabla ya hapo wanawake ndio walikuwa wakijitahidi kusubiri na kuifanya ngono au kushiriki tendo hili baada ya kuolewa tofauti na wanaume kwani wengi walikuwa wakioa wanawake bikira baada ya wao kuwa na uzoefu kitu ambacho mimi nakiona kama dhuluma (hihihihihihihi....ndio je!).
**Sababu kubwa inayotufanya ngono ifanywe kabla ya ndoa.
Tofauti na miaka ile, sasa vijana wengi wake kwa waume tunaamua kurekebisha maisha kwanza alafu ndio ndoa ifuate, sasa unapofikia umri mkubwa wa miaka 24 mpaka 35 inakuwa ngumu sana kwako wewe kuendelea kutafuta maisha kielimu na kiuchumi na kuidharau mahitaji yako ya mwili na roho (ngono na mapenzi) ambayo katika kipindi hiki ndio hupamba moto (minyenyere mpaka kwenye kope na moyo nao unahitaji kujazwa mapenzi).
Hapa ndio wengi tunaamua kuwa na wapenzi wa kudumu na kuifanya ngono kama ifuatavyo (kwa uhuru) hali inayotufanya wengi tutulie kiakili na baada ya hapo kufunga ndoa ili tuweze kushirikiana na kufanikisha malengo yetu kama wapenzi na mungu akijaalia tunaongeza kizazi.
Vijana wachache wanajitahidi kuepuka mimba wakati wa mahusiano yao ya kimapenzi ili kutosababisha watoto nje ya ndoa wakisubiri kutekeleza tukio hilo muhimu ktk maisha ya kila mwanadamu hasa wale wanaoendeleza Imani zao za kidini.
Ufanyaji huu wa ngono unaitwa ngono kabla ya ndoa ambao ni tofauti na ngono nje ya ndoa(kuchoropoka/cheating).
Natambua wengi huwa mnachanganya hapa!
Ikiwa unalolote unataka kuongezea kuhusiana na nilichokisema kwa faida ya wasomaji wengine, usisite kufanya hivyo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment