Mwanamke Anapenda Kupendwa! Mara Nyingi Wanawake Ndiyo Hasa
Huwa Na Mapenzi Ya Dhati Zaidi Kuliko Wanaume. Mwanamke Anapoamua Kuwa
Na Mpenzi Wake, Humpenda Kwa Moyo Wake Wote, Hivyo Hupenda Kuwa Salama
Katika Penzi La Dhati Kwako. Anapenda Uhuru, Anapenda Kujisikia Wazi
Kwako Mahali Popote.
Mwanamke Anajisikia Vibaya Sana Anapokuwa Hana Uhuru Hata
Wa Kukushika Mkono Mnakuwa Barabarani Pamoja. Anapenda Penzi La Uwazi!
Maana Mwingine Utakuta Akikutana Na Rafiki Yake, Badala Ya Kumtambulisha
Vizuri Kama Mpenzi Wake, Anaanza Kupatwa Na Kigugumizi. Utamsikia
Akisema: “Ah! Huyu Ni Rafiki Yangu Bwana, Anaitwa Latipha....”Hili Ni
Kosa Kubwa Linalofanywa Na Wanaume Wengi Bila Kujua Ni Kosa. Mwanamke
Anakosa Amani Ya Moyo Kutokana Na Unavyomtafsirisha Mbele Ya Rafiki
Zako. Anahisi Hayupo Salama. Lazima Atajiuliza Maswali, Kwanini
Hataki Kunitambulisha? Kwanini Anashindwa Kusema Mimi Ni
Mpenzi Wake? Sifananii? Sina Mvuto Au Nina Tatizo Gani? Hayo Yanaweza
Kuwa Maswali Yatakayomuumiza Sana Kichwa Mpenzi Wako, Ambaye Si Ajabu
Akafanya Maamuzi Ambayo Hutayapenda.
Kidonda Hiki Hubaki Moyoni Mwa Mwanamke, Huwa Vigumu Sana
Kuonyesha Wazi Kwamba Amechukia Kutokana Na Uliyomfanyia, Lakini Atabaki
Akiugulia Moyoni Mwake Kwa Uchungu. Hata Hivyo, Kinachokuja Akilini
Mwake Ni Kutafuta Mwanaume Mwingine Ambaye Atakuwa Wazi Kwake Ili Aweze
Kufurahia Mapenzi Badala Ya Kuendelea Kuumia Moyoni Mwake.
Ni Dhahiri Kwamba Uamuzi Huu Hautaufurahia Hakika.
1.
UNAVYOJALI... Mwanamke Anapenda Awe Wa Pekee Kwako, Umsikilize, Umjali
Na Umpe Kipaumbele Katika Kila Unachokifanya . Wanawake Wengi Wanapenda
Kudekezwa, Lakini Hawapendi Kuweka Hilo Wazi Kwa Mwanaume Wake. Kwa
Kumtazama Tu Utagundua Mpenzi Wako Anahitaji Nini Zaidi Kwako! Wakati
Mwingine Anaweza Kukupa Mitihani Ili Kupima Kiwango Cha Penzi Lako.
Anaweza Kukuambia Anaumwa Au Anauguliwa Na Mtu Wake Wa
Karibu, Lengo Ni Kuangalia Ni Jinsi Gani Unakuwa Makini Anapokuwa Na
Matatizo. Vile Utakavyochukulia Tatizo Lake Kwa Ukaribu, Uchungu Na
Kuona Kama Lako, Ndivyo Utakavyomfanya Aone Thamani La Penzi Lako Kwake,
Ikiwa Vinginevyo Basi Humuacha Na Machungu Moyoni, Huku Akijutia Kuwa
Na Mpenzi Wa Aina Yako. Hii Ni Siri Ambayo Si Rahisi
Mwanamke Wako Akueleze Moja Kwa Moja. Atatumia Lugha Ya
Ishara Kuonesha Jinsi Ambavyo Anahitaji Kuwa Wa Pekee Kwako. 2. JIFUNZE
SIRI HIZO..... Hapa Ndipo Mwanaume Mwerevu Anatakiwa Kuwa Makini, Ni
Lazima Ufahamu Siri Zilizopo Moyoni Mwa Mpenzi Wako.
Jifunze Kusoma Hisia Za Mpenzi Wako Kwa Nje, Kabla Ya
Kufanya Kitu, Fikiria Mara Mbili, Lakini Baada Ya Kufanya, Msome Kupitia
Uso Wake. Analifurahia Au Umemchukiza? Ni Vizuri Kugundua Hilo Ili
Uweze Kufunga Hisia Za Kumfanya Aanze Kufikiria Kukusaliti. Hata
Mnapokuwa Faragha Ni Vizuri Kuwa Makini Na Kila
Unachokifanya! Chunguza Kama Anafurahia Penzi Lako Na
Manjonjo Yote Unayomfanyia. Kumbuka Kwamba Ni Vigumu Sana Mwanamke
Kukueleza Moja Kwa Moja Kwamba Hujamfurahisha Au Kuna Kitu Umekikosea,
Hii Husababishwa Na Hofu Ya Kuogopa Kukufanya Ujisikie Vibaya. Kwa
Maneno Mengi WEWE Mwanaume Ndiye Mwenye Kazi Ya Kuangalia Mwanamke Wako
Anapenda Nini Na Nini
Hapendi Ili Uweze Kuwa MWANAUME Wake Bora, Maana Hata Hisia
Zake Za Ndani Utakuwa Unazifahamu. Ni Rahisi Sana, Soma Kupitia Macho
Yake Kila Unachomfanyia, Utaujua Ukweli. Unajua Hata Ukimwita Kwa Jina
Ambalo Hana Msisimko Nalo Lakini Ukiwa Unamtazama Usoni Ni Rahisi Sana
Kugundua Kitu Fulani, Kama Hajakipenda Utaona Kwenye Macho Na Akikipenda
Pia Utaona.
Unapokuwa Naye Faragha, Tumia Uwezo Wako Wote, Lakini
Kumbuka Kwamba Si Kila Utakachokifanya Utamfurahisha. Hii Inamaanisha
Kwamba, Baada Ya Kumchunguza Jinsi Anavyosisimka, Utaweza Kugundua Wapi
Kuna Msisimko Zaidi Kuliko Sehemu Nyingine. Hapo Sasa Unaweza Kuibuka
MSHINDI Maana Utakuwa Umeziweka Siri Zake Hadharani, Kwa
Maneno Mengine Kama Yeye Aliona Siri, Basi Umeweza Kuzigundua Na Angalau
Umeanza Kuzifanyia Kazi. Nawapenda Sana Rafiki Zangu, Ndio Maana
Nawapeni Mambo Mazuri Na Yenye Sifa Ili Msiweze Kusababisha Kitu
Kinaitwa..."UMENITENDA/AMENITENDA" (KUTENDANA NI DHAMBI KUBWA SANA
No comments:
Post a Comment