Mwaka mpya mambo mapya.
Katika tukio linaloweza kuitwa kama ndoa ya karne, mzee mmoja mwenye umri wa miaka 91, Nkwabi Ngobola Kapimbi, wiki iliyopita alifunga pingu za maisha na mkewe Maria Mkiwa (78) mbele ya mchungaji Thobias Shilole wa Kanisa la Maombezi huko Kibaha mkoani Pwani.
Katika tukio linaloweza kuitwa kama ndoa ya karne, mzee mmoja mwenye umri wa miaka 91, Nkwabi Ngobola Kapimbi, wiki iliyopita alifunga pingu za maisha na mkewe Maria Mkiwa (78) mbele ya mchungaji Thobias Shilole wa Kanisa la Maombezi huko Kibaha mkoani Pwani.
Mzee Nkwabi akipozi na mkewe Maria.
Tukio hilo lililovuta hisia za watu wengi, lilitokea baada ya
wanandoa hao kutimiza miaka 55 tokea walipoanza kuishi pamoja, katika
uhusiano ambao walibahatika kupata watoto saba, wajukuu 78 na vitukuu
24.
Akiwa amevalia suti huku mkewe akiwa ndani ya vitenge, mzee Nkwambi
alisema amejisikia furaha sana kufanya kitendo hicho kwani ni jambo
ambalo kwake na la tatu kwa umuhimu, mengine yakiwa ni kuzaliwa na kifo.
Sherehe baada ya ndoa ikiendelea.
“Nimefurahi kufunga ndoa, tukio hili ni muhimu kwangu, umri wangu ni
miaka 91, nimezaliwa mwaka mmoja na Nyerere, mke wangu ana miaka 78,
tulionana kwa mara ya kwanza mwaka 1958, tukio hili limefungua ukurasa
mpya wa maisha yangu, najua Mungu yuko pamoja nasi, nina wajukuu 78 na
Vitukuu 24.
“Watu wengi wanauliza tulikuwa wapi siku zote hizi, ni kwamba
nilikuwa simuamini sana mke wangu, tulikuwa tukikorofishana lakini bado
tuliweza kudumu. Mungu ni mwema sana,” alisema.
Alisema hajali kama kuna watu watakuwa wakizungumza wanalojua kuhusu ndoa yao, lakini anachofurahi yeye ni kufunga ndoa na mke wake anayempenda.
“Mara ya kwanza mke wangu alikuwa anasita, lakini nilisema lazima
tukafunge ndoa kwenye kanisa la Mzee wa Upako ( Antony Lusekelo),
nampongeza mchungaji Thobias Shilole kwa kuwa pamoja nasi na kukubali
kubariki ndoa yetu, lilikuwa jambo la furaha kwangu na mke wangu,”
alisema Babu Nkwabi.
Kwa upande wake, mkewe Maria alisema awali alikuwa akisita kwa kuona
kama itakuwa ni kituko mbele ya jamii, lakini baada ya majadiliano na
mumewe, akaridhia jambo hilo kwa moyo mmoja.
“Najua maneno lazima yasemwe lakini mimi nampenda sana mpenzi wangu,
tuliwahi kupitia mambo magumu, milima na mabonde lakini leo tumeamua
kuzishinda hila za muovu ya shetani, si kitu cha kawaida kufunga ndoa
kwa umri wetu lakini Mungu ndiyo njia ya kweli na uzima,” alisema mama
huyo.
No comments:
Post a Comment