kuna wanawake jamani humu mjini mimi wananiudhi yani mwanamke anapenda pesa mbele kuliko hata ubinadamu..
jamani
wanawake japokuwa mnapenda sana pesa lakini kaeni mkijua ya kwamba kuna
siku mtu anapata na kunasiku mtu anakosa tena anaweza kukosa wiki nzima
mfulululizo sasa wewe ndio kutumia akili yako ya ziada kumpa moyo mumeo
au mchumba wako
basi bwana kuna dada mmoja hivi mtoto mdogo tu labda sasa hivi anamiaka 24 nilimjuaga kipindi cha nyuma huko..
huyu
dada alikuwaga anamwanaume wake mmoja hivi huyo kaka alikuwa mzuri
jamani yani kwanza ni mcha MUNGU, pili ni mzuri wa sura, tatu alikuwa
anajipenda yani akivaa unaona eeehhh sasa mwanaume si ndio huyu..
huyu
kaka wa watu yeye alikuwa anakazi yake ya kawaida tu kama mtu wa IT
katika ofisi fulani ya wahindi huko kama mnavyojuwa wahindi nao hawalipi
vizuri kiivyo yani kijana hakukosa hela ya kula, kuvaa, wala kulipa
kodi ila alikuwa hana ile hela ya mashauzi na kuhonga saaana..nadhani
mnanielewa
basi
maisha yakaendelea kumbe yule dada alikuwa yupo na huyu kijana lakini
pembeni anamwanaume mwengine yupo mgodini huko ana hela zake anamuhonga
anaishi mjini kijana wa watu akawa anajua zile hela dada anatumiwa
kutoka nyumbani asijue ya kwamba shoga anahongwa na kidumu
maisha
yakaendelea hivyohivyo bwana unaambiwa iba tu ila siku yako ya
kukamatwa ikifika utaumbuka basi siku hiyo shoga kamuaga bwana kwamba
anaenda kwa ndugu yake iringa kumbe shoga kaenda geita huko kwenye
migodi kwa bwana..
huwa
yule bwana anamtumia hela ya kwenda na kurudi pamoja na ya kukaa
hotelini kwahiyo akiwa kule yule bwana analala hotelini na shoga mpaka
mdada akiondoka huyu bwana yeye hajaoa
basi
bwana shoga siku hiyo kapelekwa ubungo na jamaa wakaagana vizuri dada
akaondoka zake kwa hawara yake akafika mwanza kama kawaida anahoteli
anayofikiga na wanamjua akakodi chumba akaingia kujipumzisha kabla bwana
hajaja
basi
jioni bwana kaja wenyewe wakalala vizuri asubuhi yake bwana akaaga
kwamba anaenda kazini atarudi jioni na kwakuwa ilikuwa ijumaa wakapanga
kwamba usiku wataenda kula sehemu halafu waende club
basi
jioni ikafika jamaa kaja ameshavaa, shoga tena naye ndio kuulamba tena
bonge la kimini (namwaga razi miye geita atanijua nani) sijui hii nyimbo
mnaijua...basi haoooo mpaka sehemu moja ya kula nyama huwa wanachoma
sana nyama na watu kunywa pombe
wakakaa
pale kula, wakaja na marafiki wa jamaa wanaofanya wote kazi na wanawake
zao basi wakalewaaa na kula mara wakaja wadada wawili wanaofahamiana na
hao majamaa wakawa wamekaa meza ya pili wanakunywa jamaa kwakuwa
anawajua akaamua kuwaita wakae meza moja wanywe pamoja
basi
jamaa yeye na wenziye si wanahela basi wakawa wanazungusha tu round
hata kwa wale wanawake waliokuja yani hawajanunua beer hata moja
wananunuliwa tu, basi dada akawa ananihadithia nilivyoona vile da Rose
nilikuwa natoa macho hawa wanawake wasije wakawa ni mahawara wa huyu
bwana mbona anawafanyia hivyo
basi
bwana walivyolewa vya kutosha wakaamua kwenda club sasa yule bwana
akawaambia wale wanawake twendeni wote club tukamalizie siku shoga tena
wale wanawake wakatae ofa haooo na wengine mpaka club
sasa
bwana kufika club watu wanacheza wanafurahi shoga akaenda chooni maana
tena siunajua ukinywa beer ishu yake ya kwenda chooni kila saa
basi
shoga kutoka chooni anamkuta yule bwana anacheza na mwanamke mmoja
katika wale waliokuja nao anamshika kiunoni na kumbusu kwenye
shingo!!!!!!!
yaani
ananiambia dada nilitaka nife nilishikwa na hasira kilichokuja
akilini mwangu ni kwenda duka la jirani pale kununua wembe..simnajua
haya maduka karibu na disco huwa hayafungwi mapema hata pale billicanas
lipo moja
shoga
kuchukua kiwembe kwenda kuanzisha ugomvi na yule dada, yule dada kutaka
kumpiga na mwenziye shoga kuchukuwa kiwembe kuanza kumchanjachanja yule
dada, chanjaaa ile mbaya yule bwana kuona vile akamchukua yule dada
wakaondoka kurudi hotelini kukimbia soo
waliporudi
sasa ndio ugomvi tena ukaanza hotelini shoga kugombana gombana na wewe
akaanza kukandwa maana yule dada na mwenziye pia walimpiga sana haswa
usoni akawa ameviria kama damu na kesho yake alikuwa ndio arudi dar
na
asingeondoka kesho yake lazima yule dada angemfwata jamaa agombane na
kutaka kuonyeshwa yule msichana yuko wapi walipize kisasi
basi
kesho yake asubuhi huyoo kwenda stand kuchukua bus kurudi dar..ubungo
huku yule bwana yake anamsubiri kwa hamu tena siunajuwa mtu ukisafiri
ukiwa unarudi sasa hayo mahamu ya mapenzi
alivyofika
dar bwana kumuona vile akaanza kumuhoji kulikoni huko umegombana na
ndugu zako ama vipi? basi dada akatoa visingizio kibao ambavyo bwana
bila kujuwa kuwa ni uongo akakubaliana navyo
basi
wakaendelea kuishi jamani ya mwizi arubaini yule msichana sijui alipata
wapi number ya shoga akampigia simu siku hiyo usiku wakiwa wamelala na
bwana yake shoga si hajui number akamwambia mpenzi wake huyu sijui nani
ananipigia sasa hivi na number ni ngeni siijui bwana akasema ngoja
nipokee
loooooooooo
anajuta mpaka leo...shoga sindio kuanza kuchamba yani hajasubiri hata
kusikia hallo yani simu alivyosikia tu imepokelewa ni matusiii kumtukana
demu tukana na jamaa kakaa tu kimya hakutaka kukata simu demu
akamalizia natulivyokupiga bado hiyo ole wako ukanyagi huku tena
utajuta..akakata simu
ndio
bwana sasa kukata simu na kuanza kumuhoji vizuri shoga na mwanaume
asijue unamwanaume mwengine nje utajuta...shoga ugomvi huku ukaanza tena
wa haja shoga kesho yake akaambiwa apaki kilichochake aondoke
ndugu
kashaharibu kotekote atafanyaje sasa na ndugu zake wako mkoani basi
akaomba msamaha lakini yule bwana alikuwa na hasira sana na hakutaka
kumuona tena
alikasirika
kwasababu ya yeye kuwa na mtu nje na kisa ni kwamba alikuwa anahongwa
hela..kwanini hukuweza kunivumilia??? basi shoga akalia na kuomba
masamaha pale omba omba na wewe mwishoe kweli alisamehewa na hakufukuzwa
tena
basi maisha yakaendelea kama kawaida japo sasa huyu mwanaume alianza kumchunga sana na kumchunguza kila anapoenda na anachofanya
lakini
bwana hulka ni hulka tu japo alisamehewa bado alitafuta mwanamme
mwengine nje mwenye hela na kumuhonga tena sasa hivi ndio akapata wa
hukuhuku dar mwanaume anayejiweza mara mbili ya huyo aliyekuwanaye na
alikuwa anaishi tu mwenyewe hajaoa wala hana mtoto
mwanamke
akaendelea kula huku na kule bila hata kujali na alikuwa anatumia line
nyengine ambayo huyu bwana haijui sasa basi mapenzi kule kwa bwana
mwengine yakawa motomoto wanakula bata tu siku nyengine anaaga anasafiri
kumbe haendi popote anajifungia nyumbani kwa yule bwana wiki nzima
anaenjoy tu
basi
mwishoe akaona sasa huyu wa zamani anamzingua tu siku hiyo akarudi
nyumbani na kumueleza kwamba hamtaki tena atafute mwanamke mwengine
amechoka kuishi na mtu asiyekuwa na hela za kumuhudumia
ipasavyo..huyoooo akaondoka
akaachana
naye na kuhamia kimoja na yule bwana mwengine, basi maisha yakasonga
MUNGU akambariki yule kaka aliyeachwa akapata mwanamke mwengine na muda
si mrefu akaoa
basi shoga alivyosikia jamaa kaoa akaanza kuchamba na aoe tu miye maisha ya shida siyataki na siyawezi
mapenzi
tena kwa bwana mpa yakawa motomoto mpaka akaamua kumzalia na mtoto
mmoja wa kike maisha tena ndio yamepamba moto kwa maraha shoga akawa
anahisi kama yupo angani yani anajisikia hatari chini hakanyagiki
baada
ya mtoto kufikisha mwaka yule bwana likatokea tatizo kazini akafukuzwa
sasa maisha ndio yakaanza kuwa magumu hakuna mfano shoga akaanza kuona
junejuly
basi
alivyoona zile raha hamna tena saa zingine hawana hata kitu cha kula
wanakoroga uji au mpaka jamaa akaombe chakula kwao ndio wale akasema
sasa amechoka alichofanya ni kubeba mwanae na kila kilichochake na
kuondoka
yule bwana akambembeleza na kumuomba arudi kwamba atatatfuta kazi lakini mwanamke hakuwa anataka kusikiliza kitu miezi ikaenda
siku
bwana jamaa akapata kazi sehemu nyengine, mwezi, wa pili, wa tatu jamaa
akapata na mwanamke humohumo ofisini kwao wakawa wote wanaendelea na
maisha yao
looohhh jamaa sasa anaoa JUMAPILI hii ya keshokutwa
yani
yule msichana kusikia story ya jamaa kachanganyikiwa yani analia kama
mtoto mdogo ananipigia simu anasema dada nimekosa ndoa ya
pili..nikamwambia wee nitolee upumbavu wako nikamkatia na simu sitaki
kabisa anililie miye nilimuonya tokea mwanzo usipofunzwa na mama yako
utafunzwa na ulimwengo haya cheza sasa segere ulimwengu unaokupigia
No comments:
Post a Comment