Kiongozi wa kanisa Katoliki papa Francis ambaye
ameahidi kutovumilia vitendo vya udhalilishaji wa kingono
tangu ateuliwe kuwa kiongozi wa kanisa hilo Machi
mwaka jana, amesema kashfa hiyo ni aibu kwa kanisa.
Papa Francis ameyasema hayo wakati wataalamu wa
Umoja wa Mataifa wakiwahoji wajumbe wa kanisa hilo
juu ya udhalilishaji kingono wa watoto uliofanywa na
viongozi wa dini. Papa Francis amesema kuna kashfa
nyingi ambazo asingependa kuzitaja binafsi , lakini
amesema kila mmoja anazifahamu. Amesema hayo
katika misa ya asubuhi katika kanisa la Santa Marta leo.
Wakati huo huo kanisa Katoliki limesisitiza leo kuwa
lina nia ya kufikisha mwisho udhalilishaji wa kingono
unaofanywa na viongozi wa kanisa hilo, wakati
wajumbe wa ngazi ya juu wa kanisa hilo wakihojiwa
mbele ya jopo la kamati ya kulinda haki za watoto la
Umoja wa Mataifa.
No comments:
Post a Comment