Tuesday 7 January 2014

HILI NDILO....TUKIO 2013 LILILOCHUKUAA REKODI...ZAIDI EWE NDUGU MSOMAJI WANGU NI WAJIBU WAKO KUMSHUKURU M/MUNGU ALIYEKUUMBA KWA KUKUPA AFYA NJEMA ULIONAYO, KWANI KUNA WANAOTESEKA KAMA HUYU HAPA.. HADI HURUMA


Wakati mwingine binadamu huwa tunajisahau kumshukuru Mungu kwa afya nzuri aliyotupa bila kujua kuwa wapo watu duniani wanaoteseka mno. Mwanaume huyu wa nchini Indonesia ambaye mwili wake umefunikwa na upele mkubwa ameiomba dunia imsaidie kumponya tatizo lake ambalo sasa limesababishwa ashindwe kuona vizuri baada ya madude hayo kufunika macho yake.




Slamet, anayetokea East Java, anaaminika kuwa na ugonjwa uitwao neurofibromatosis. Kwa mujibu wa kaka yake, Suwadi, ndugu yake huyo mwenye miaka 59 aliondolewa kitu kama jipu kwenye kiuno chake mwaka 1991. Lakini miezi sita baadaye vipele vingine vikaanza kutoka usoni na kwenye mwili wake.




Miaka kadhaa baadaye hali hiyo imekuwa isiyovumilika kwakuwa Slamet husikia maumivu mwilini muda wote. Majipu hayo kwa sasa yamekuwa mengi kiasi cha kuziba pua zake na kumfanya apumue kwa tabu.



No comments:

Post a Comment