Sunday, 19 January 2014

MICHEZO:Manchester yanyolewa 3-0 na Chelsea

Kocha wa Chelsea Jose Mourinho amesema kuwa matumaini ya mabingwa watetezi wa ligi kuu ya Premier, Manchester United ya kulihifadhi kombe hilo msimu huu yametumbukia nyongo, baada ya klabu yake kuishinda United kwa magoli matatu kwa moja.


Nyota wa Cameroon, Samuel Eto'o aliifungia Chelsea magoli yote matatu na kuandikisha historia yake ya kufunga magoli matatu katika mechi moja ya ligi kuu ya Premier.

Chelsea hata hivyo imesalia nafasi ya tatu alama mbili nyuma ya Arsenal na moja nyuma ya Manchester City.

Mourinho amesema itakuwa rahisi kwa ngamia kuingia tundu la sindano kuliko Manchester United kushinda taji la ligi kuu msimu huu.

'' Ni vigumu sana. Wao wana alama kumi na nne nyuma ya Arsenal, kumi na tatu nyuma ya Manchester City na kumi na mbili nyuma yetu'' Alisema Mourinho.
''Pengine timu moja isambaratike, lakini kwa timu tatu kusambaratika kwa pamoja, itakuwa vigumu sana. Nadhani kilichosalia ni wao kupigania kumaliza katika nafasi za kwanza nne'' Aliongeza Mourinho.

Kadi Uwanjani
Nahodha wa United Nemanja Vidic alipewa kadi ya njano muda mfupi kabla ya mechi hiyo kumalizika, baada ya kumfanyia madhambi Eden Hazard, naye Rafael da Silve akaonyeshwa kadi ya njano kwa kumjeruhi Gary Cahili dakika moja baadaye.

Hata hivyo kocha wa Manchester United, Moyes, alihisa kuwa refa wa mechi hiyo alichukua uamuzi mkali zaidi kwa kuumpa Vidic kadi nyekundu moja kwa moja, huku akikiri kuwa Rafael alikuwa na bahati sana pale refa alimpa kadi ya njano badala ya kadi nyekundu.

Naye Mourinho alimsifu Eto'o mwenye umri wa miaka thelathini na mbili, licha ya kuwa aliwahi kumshutumu kuhusiana na matokeo yake hasa baada ya kuwasili kutoka klabu ya Anzhi Makhachkala mapema msimu huu.

 
Jose Mourinho aamini Manchester United itaambuliwa patupu msimu huu

No comments:

Post a Comment