Kikongwe
mwenye umri kati ya miaka 85 hadi 90 ambaye bado hajafahamika jina lake
amekutwa katika kijiji cha Nyashimbi kata ya Muhongolo wilayani Kahama
Mkoani Shinyanga kwa kile kinachodaiwa kuwa huenda ni mchawi aliyeanguka
usiku wakati akiwa kwenye safari zake angani.
Kikongwe huyo baada ya kufikishwa kituo cha polisi
Kwa
mujibu wa wakaazi wa Kijiji hicho bibi huyo ameonekana leo majira ya
saa 12 asubuhi akiwa katika vichaka vilivyo kando ya barabara na
alipoulizwa aliongea kidogo tu kuwa anatoka Kijiji cha Nyihogo wilayani
Kahama.
Kikongwe huyo akiwa chini huku amezingirwa na kundi la wananchi
Akiwa amelala chini kwa kile kinachodaiwa ni njaa
Alipoendelea
kuhojiwa alisema alikuwa na wenzake na vitu mbalimbali ila wamemuacha,
huku akisema hawezi kuongea zaidi kwani anahisi njaa kwakuwa alikula
toka jana tena chakula Kibichi, jibu ambalo liliwashangaza wengi ni aina
gani ya chakula ambacho huliwa kikiwa kibichi.
Bibi
huyo amekutwa na nguo moja ya Kimasai na nguo zingine chache za kawaida
lakini hakukutwa na vitu vyovyote vinavyoashiria kuwa huenda ni mchawi,
hivyo kuleta hisia kuwa huenda alikuwa ni mtembea kwa miguu tu
aliyepotea njia kwani watu wote wa eneo hilo hakuna anayemtambua.
wananchi wakimwangalia bibi kizee huyo akiwa hio bin taaban
bibi kizee huyo akiwa ameanguka chini usiku wa kuamkia leo
No comments:
Post a Comment