Tunakabiliwa na janga. Faru wanauawa na maharamia kila baada ya
dakika 10 na ni wachache kuliko chui 3,500 ambao wamebaki porini.
Hili siyo tatizo tu la kimazingira. Kwa tembo
25,000 kuuawa mwaka 2011 na 22,000 kuuawa mwaka 2012, ni ishara
inayoonyesha kuwa biashara haramu ya wanyama pori sasa imekuwa ni
uhalifu wa kidunia wenye nguvu ya kuathiri maendeleo ya kiuchumi,
kusababisha migogoro, kuimarisha vikundi vya kigaidi na kuathiri watu
wenye hali duni ya watu waishio katika umaskini.
Ujangili unaathiri jamii barani Afrika, hususan
yale maeneo katika bara ambapo wanakabiliwa na hali mbaya ya janga la
ujangili. Kuna kazi muhimu inaendelea kila siku katika bara zima
kushughulikia; kuanzisha jitihada za uhifadhi nchini Namibia au uzoefu
wa kiteknolojia mpya nchini Kenya.
Kazi hii imekuwa na athari mbaya kwani zaidi ya
askari wa wanyamapori 1000 wamekwisha uawa ndani ya kipindi cha miaka 10
iliyopita. Afrika inaongoza katika mwitikio wa kisiasa kwa hatua
zilizochukuliwa katika Mkutano wa Afrika juu ya tembo mwishoni mwa mwezi
Desemba mwaka jana (2013) sambamba na jitihada za Gabon katika kuliibua
hili katika Umoja wa Mataifa.
Uongozi ulioonyeshwa na Botswana, Gabon na nchi nyingine ndivyo haswa inavyohitajika kulikabili na kulimaliza tatizo.
Lakini ujangili na biashara haramu ya wanyamapori
ni suala linaloigusa dunia nzima. Biashara haramu ya wanyamapori ni
mtandao wa kutisha wa kiuhalifu ambao una thamani ya mabilioni na ina
fursa ya kuyumbisha ukanda na kutishia ustawi wa kimaendeleo endelevu.
Hatupaswi kuiachia Afrika ikabiliane na tatizo
hili bila kuwasaidia. Lazima wote tuonje madhara ya uhalifu wa
wanyamapori kuanzia usafishaji wa fedha haramu hadi kuharibu mazingira.
Ni jukumu letu kusaidia uongozi ambao nchi za
Kiafrika na kwingineno wanaonyesha juu ya suala hili. Hivi karibuni,
tumeridhia Mpango Kazi katika Serikali namna ya kukabiliana na biashara
haramu ya wanyamapori.
Pia tumetangaza ruzuku mpya za thamani ya paundi
milioni 10 kwa miradi ambayo inalenga kukabiliana na ujangili wa tembo
na biashara nyingine haramu za wanyamapori na tutatoa taarifa kwa kina
baada ya kufahamu mfumo tutakaotumia kutoa ruzuku hizi.
Mnamo Februari 13, Uingereza ilikaribisha Serikali
mbalimbali za Afrika, Asia, Amerika na Ulaya kuleta juhudi za pamoja za
kimataifa.
Tanzania ilikuwa nchi yenye uwakilishi wa kipekee
kwa kuwakilishwa na Rais Jakaya Kikwete, Waziri wa Mambo ya Nje, Benard
Membe na Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu. Hili ni jambo
lililoleta hamasa na kuonyesha dhamira imara na umakini wa Tanzania
katika kushughulikia tatizo la ujangili.
Waziri Nyalandu mnamo Februari 8 mwaka huu (2014)
alisema; “Ukizingatia uzito wa tatizo la ujangili linaloikabili
Tanzania, Serikali imedhamiria kupambana na kuushinda ujangili”.
No comments:
Post a Comment