Yawezekana
ikaonekana kama ni jambo dogo sana kushukuru lakini shukrani ya kweli
kwa mtu mzima kama wewe sio tuu kusema ahsante, bali shukrani ina maana
ya kuwa:-
1. Umethamini ulichopewa
2. Umeiona hisani au huduma ya mtu husika
3. Unatambua kuwa ni jambo jema limekutokea kwamba mtu fulani kakupatia kitu au huduma fulani. Ni kama vile kujinyenyekeza
kimoyo moyo na kujiambia kuwa pengine wala haukustahili kufanyiwa hivyo
ulivyofanyiwa, au kupatiwa hivyo ulivyopatiwa bali ni kwakuwa imekuwa
jambo la kheri kwako kupata ulichopata.
Maana
hiyo ya shukrani sio tuu kwamba kwa wale wanaokusaidia au kukupatia
vitu BUREE, bali hata kama unalipia , bado unahitaji kushukuru kwani
wapo wengi wanaolipia huduma au bidhaa na bado wasipate huduma nzuri au
wasipatiwe kile wanachohitaji.
Swala
la ahsante sio tuu kwenye biashara. Ahsante ni swala la msingi hata
katika mahusiano -mume inabidi amuambie ahsante mke, na mke kwa mume pia
kwa sababu hizo hizo.
Watoto kwa wazazi pia.Wanafunzi kwa walimu n.k
Hata
kama ni mzazi, mwalimu au mpenzi amekutendea jambo jema, usijione kuwa
ni eti ulikuwa na haki ya kutendewa hivyo ulivyotendewa hivyo basi hauna
haja ya kushukuru.
Kushukuru
kwako kwa ufasaha bila kusanifu, kunamgusa mtu husika hivyo kuna
muandaa au kumpa hamasa ya kukutendea jambo jema lingine. Ndio maana
wanasema KUSHUKURU NI NAMNA NYINGINE YA KUOMBA.
Utaona
kuwa shukrani sahihi inakufanya uthamini ubinadamu, shukrani sahihi
inakufanya ujitambue vema na kukumbusha kuwa una thamani kwani mtu
mwingine amekujali kufanyia hicho ambacho unasema ahsante.
--Mara
baada ya kusema hivyo, napenda niseme ahsante kwako msomaji wa Mbuke
Times. Uwepo wako na support yako inanipa nguvu ya kutafakari mambo kila
siku. Mie pia ninanufaika.
No comments:
Post a Comment