Thursday 6 February 2014

KABLA YA KUACHANA NA MPENZI WAKO WA SASA NA KUJIPELEKA HUKO UENDAKO, TAFADHALI SOMA RASIMU HII


1. Jipe nafasi ya kutosha kutafakari kama ni kweli sasa hana maana tena hata kama amekukera.


2. Chunguza kwa makini kama kuna hali inayomfanya kuwa hivyo na jaribu kumsaidia aitatue na awe kama mwanzo


3. Orodhesha kila baya na jema na ona upande upi umezidi na hata mmoja ukielemewa angalia wewe umechangia upande upi katika hayo.

4. Kumbuka mahusiano ya kimapenzi sio sawa na mchezo wa ngonjera ambao una wimbo wa kuingilia na wa kutokea. Usitoke na wimbo wa mbwembwe nyingi za kumponda halafu baada ya kuumizwa huko uliko ukaanza kuutafuta wimbo wa kumrudia

5. Mapenzi ni kupitia changamoto na vikwazo mbalimbali mkiwa pamoja na kisha kuyatatua kwa pamoja.

6. Shetani unayemjua ni bora kuliko malaika usiyemjua. Hapa kumbuka hakuna mahusiano yasiyo na matatizo yake hivyo vumilia ulipo.

7. Mapenzi ya mwazo huwa na kila aina ya furaha ingawa ni wachache wanaoweza kubakia na hali hiyo hivyo kuwa na msimamo hapo ulipo

8. Kama unahitaji furaha na mahaba ya dhati anza kwa kutengeneza hapo ulipo usije tegemea kuwa kuna mtu atakupa furaha kabla ya wewe kuitengeneza furaha hiyo.

9. Ushawishi wa zawadi na fedha sio mapenzi kwani hata changudoa siku hizi wanatoa zawadi za pipi ukiwachukua lakini wao wanatengeneza mazingira ya kukukamua hela vyema hivyo ikubali hali yako.

10. Hakuna hali inayodumu, kama unamkimbia kwa kuwa ni maskini au ana maswahiba yake binafsi kumbuka hayo ni mapito na baada ya kila usiku mchana nao huja na mambo mapya.

La ziada, kama ukiona umeshindwa haya yote basi wewe rudia kusoma tena na tena na kuongeza yako mpaka mrudiane na ikishindikana wewe soma tuu

No comments:

Post a Comment