Monday, 10 February 2014

MAMBO MUHIMU YA KUZINGATIA UNAPOKUWA NA RAFIKI KATIKA MAISHA YAKO.....

1. Usiwe mwepesi wa kutoa lawama na kumhukumu kwa kila jambo ila jaribu kumwelewa na kumfanya akuelewe wewe pia


2. Usijifanye kuwa wewe ni wa muhimu kuliko yeye ila amini yeye ni wa muhimu zaidi jambo litakalo mfundisha nae kukuona wa muhimu


3. Kuwa karibu na matatizo yake hata kama huna uwezo onyesha kuwa wewe ni bega lake litakalo mfuta machozi wakati akilia yaani mpe ushauri wenye utatuzi na ajivunie wewe

4. Usiwe mwepesi wa kuropoka kwa watu mapungufu yake ila jitahiti kuwa mwazi kwake na kumbadilisha ikibidi

5. Jaribu kuwa msiri wa kutunza mambo yanayowahusu na kutoyashirikisha kwa wengine

6. Usiwe mwepesi wa kumkatisha tamaa kwa kila jambo.

7. Epuka kuwa mzigo kwa mwenzako nawe jitume na kuonyesha mwenzio anaweza kukutegemea pia

9. Vumilianeni kwa mambo yanayoweza kuwafanya mwonekane kutofautiana na jaribuni kuyamaliza mambo yenu wenyewe.

10. Furahia mafanikio ya mwenzako toka moyoni na chukua kama changamoto za kujifunza nawe ufanye vyema kuliko kuanza kujenga uadui au kumsema vibaya.

11. Jitahidi kuzuia hasira zako zikufanye utoe maamuzi utakayoyajutia baadae.Fanya maamuzi kwa busara katika kila jambo.

12. Jenga tabia ya kuwasiliana na rafiki yako mara kwa mara kama yuko mbali na hata kama mnakaa pamoja

13. Marafiki wema pia huletwa kwa neema ya Mungu hivyo mwombe Mungu marafiki na kumshukuru kwa kuwapata na mwombe akupe hekima na uvumilivu wa kuishi nao

Kitu cha muhimu zaidi ni kwamba kuwa na rafiki mpya kila siku ni rahisi sana. Ila ugumu ni kuweza kubaki na marafiki hao milele.

Hivyo ni vyema kujenga tabia ya kuheshimu uhusiano wa kirafiki na kuilinda.



No comments:

Post a Comment