Fans,
Alhamis njema
1.
Umeshawahi kumuomba mtu kitu halafu yeye akakuahidi vizuri ila asikutimizie, na
wala asikuambie kuwa haiwezekani bali
kwa namna mambo yanavyoenda tuu utajua kuwa mtu huyo hatokusaidia.
2. Je
umewahi kumdai mtu ikafikia mahali ukimtafuta kwa simu hapokei , hapatikani au
simu inakatwa, anazima, ukimuandikia
message hajibu, na emails zako ndio kazichunia kabisa.
Basi
sikiliza:
Matendo
hayo hapo na yanayofanana na hayo yanasababishwa na kasumba ya watu kudhani
kulikimbia tatizo ni kulitatua. Wengi wanaogopa kukabiliana na tatizo, kujadili
na yule ambaye wanadhani wamemkosea au tuseme yule ambaye ataumia au ameumia
kutokana na maamuzi yao.
Unapodaiwa
halafu ukaanza kuzima simu, kutokujibu message au kutokata kuonana na
anayekudai yawezekana kabisa ukawa upo katika ugonjwa huu. Unaogopa
kujadiliana, unaogopa kuli-face tatizo.
Kumbuka kwa
namna hii hautatui tatizo, bali ndio kwanza unaliongeza kwani unaharibu
mahusiano yako na mtu husika, unajipotezea amani ya moyo na unausonga ubongo
wako kwa mambo “magumu” hivyo kuunyima uhuru wa kufikiri vema.
Kasumba hii
huanza kidogo kidogo kwa mambo madogo madogo, mpaka unajikuta hata kwa mambo
makubwa unakuwa muoga. Pengine ni malezi
uliyokulia ambapo haukupewa nafasi ya kujieleza, ulitakiwa tuu kufuata
unayoambiwa, na ilikubidi kupinga kwa namna yako isiyo ya wazi wazi, mfano
ulipotumwa kuenda kufanya shughuli fulani wakati wewe ulitaka kufanya shughuli
nyingi , ukiwa mdogo uliamua kukubali kwenda hata hivyo, hukufanya kama
ulivyoambiwa badala yake ukaishia kucheza.
Hata ukiwa
mkubwa inaendelea kwa mfano unajua wazi
kuwa hata hautoweza kufika kwa wakati katika ahadi mnayokubaliana ila unajikuta
unakubali tuu kwa kuwa unaogopa kujadili kutokuweza kwako. Unadhani hapo
unatatua tatizo kumbe ndio kwanza unalizidisha.
Mojawapo ya mbinu za kushinda hili ni :
Kuamini
kuwa ni busara zaidi kujenga mahusiano mema na watu kuliko kuogopa kuonekana
umekosea au kuliko kudhani utamuumiza mtu kwa kusema ukweli, kumbe tambua
ataumia zaidi akijua umemdanganya kuliko unavyodhani eti ataumia kwa ukweli
wako.
Usiogope hata kama umekosea. Hakuna aliyemkamilifu hapa duniani. Kama ulitaraji kwa dhati kufanya jambo fulani ila mazingira au udhaifu wako ulikufanya ushindwe kutimiza ulichotakiwa kufanya ni vema ukajielezea. Itakuletea heshima zaidi, na kukupa nafasi ya kufanya makubwa zaidi.
No comments:
Post a Comment