Sisi
binadamu namna yetu rahisi ya kuelewa na kukumbuka mambo ni kwa
kuyaweka mambo katika makundi mfano tunawagawa watu katika makundi kama
marafiki, ndugu, watoto, maadui, warefu, wafupi, n.k. Makundi haya
yanatusaidia kujenga picha ya haraka hata kama wakati fulani hatuwezi
kuelezea wazi wazi kundi husika ni nini haswa na pia kunaweza kuwa na
tofauti kati ya watu au vitu katika kundi husika.
Mtindo huu wa kutambua vitu au watu kwa makundi ndio unaopelekea pia kuwepo kitu tuiitacho kwa kiingereza PREJUDICE yaani CHUKI.
Kwakuwa
umezoea kuwaweka watu katika makundi fulani, na kuwatambua watu kwa
makundi kutokana tayari na aina ya picha ya kundi husika , basi waweza
kujikuta ukiwaweka tuu watu katika makundi na kuwatafsiri hivyo,
ingawaje sio sahihi kwani ingawaje wewe unafikiria na kutambua kwa njia
ya MAKUNDI, kumbuka kuna utofauti mkubwa kati ya mtu aliyepo katika
KUNDI na maana unayoipa KUNDI husika.
Hivyo
unaweza kumtafsiri mtu kuwa MVIVU/MWIZI/MWONGO kwa sababu tuu unamuona
yupo katika kundi fulani ambalo wewe huwaita wavivu/Wezi/waongo, ila
kiukweli huyo mtu mmoja sivyo unavyodhani.
Mara ngapi umesikia mtu
akisema "Vijana wa siku hizi wavivu", na wengine wamekosa kazi kwa
sababu tuu eti wamemaliza chuo fulani hivyo "hawana ujuzi".
CHUKI au
PREJUDICE ni pale unapowatafsiri watu wengine VIBAYA kwa sababu kiakili
yako wapo katika MAKUNDI ambayo ni mabaya. Unaamini kwa mfano kila
anayefanya biashara ONLINE ni tapeli, kila mwenye NGO basi ni tapeli,
kila MNIGERIA ni mwizi, n.k
Kumbuka ili kuzuia CHUKI ya namna hii jitahidi kufikiria na kuwaona watu kama mtu mmoja mmoja na sio sehemu ya kundi.
Kuwa
makini na namna unavyotafsiri watu kwa kuangalia UMRI , JINSIA, UTAIFA,
DINI, KABILA, AINA YA KAZI, MIJI WANAPOTOKA, MAHALI WANAPOISHI n.k
Pia jichukulie wewe ndio ungekuwa una tafsiriwa vibaya ungejisikiaje ?
No comments:
Post a Comment