Kwa
kawaida kadiri mwanaume anavyokosa tendo la ndoa kutoka kwa mwenzi wake
ndivyo ambavyo anazidi kujishinikiza kihisia. Kama atakosa tendo kwa
wiki nzima mambo huwa magumu zaidi, kwa sababu bila kujijua mwanaume
hubadilika na kuwa kama simba au chui mwenye njaa aliye tayari kumvamia
na kumjeruhi yeyote.
Nataka niwaambie wanawake kwamba, kama hujitahidi kuhakikisha kwamba,
mumeo anamaliza kiu yake, hasa kama ana kiu sana, unachofanya ni
kutengeneza mzimu ndani mwako. Mume anayekandamiza hasira za kunyimwa
tendo la ndoa na mwenzi wake anakuwa kama mzimu.
Labda niwape siri moja kuhusu athari za njaa ya tendo la ndoa kwa
wanandoa. Mkisikia au kusoma katika vyombo vya habari kwamba, mume
amemuuwa mke wake kwa sababu ya wivu wa kimapenzi, jaribuni kuchunguza.
Inawezekana kabisa, mke huyo kabla hajauawa alikuwa hampi mumewe
unyumba, hivyo kumfanya mumewe akusanye maumivu ya kihisia ya kunyimwa
unyumba na mkewe yaliyomfikisha mahali pa kugeuka kuwa mzimu uliommaliza
mkewe.
Tafiti nyingi zinakubaliana na jambo hili kwamba, kwa sababu ya uzalishwaji wa mbegu za kiume, homoni ya sili ya testosterone na
sababu nyingine, mwanaume huhitaji kufanya tendo la kujamiiana angalau
mara tatu kwa wiki ili aweze kuhisi ahueni. Labda tu pale ambapo
mwanaume anaumwa, ana matatizo ya kusongeka kiakili au muda mdogo sana,
ndipo ambapo anaweza kukaa muda mrefu bila kushiriki tendo la ndoa.
Lakini hata mkewe anapokuwa na matatizo ambayo yanamfanya asiweze
kushiriki tendo la ndoa na mwanaume anampenda mkewe, anaweza kabisa
kuratibu hisia zake na kumudu kuvumilia.
Lakini kama inatokana na mwanamke kutojisikia kufanya na kama
mawasiliano kuhusu jambo hilo hayajawa wazi, mwanaume hugeuka kuwa mzimu
kweli. Kumbuka kuna migogoro mingi sana ndani ya ndoa ambayo chanzo
chake ni tendo la ndoa, ingawa wanandoa wanakuwa hawaoni. Wanaume
wanahitaji tendo la ndoa zaidi kuliko wanawake na hiyo haina maana
kwamba, ni wahuni au wazinzi, hapana. Kama mwanamke atajitahidi kuwa
kiongozi wa jambo hili na hasa kufungua milango ya mwasiliano, yeye
ndiye atakayenufaika zaidi.
Mwanamke anapaswa kukumbuka kwamba, hamu ya mwanaume kwenye tendo la
ndoa ni kama mwito wa kimwili kama ilivyo njaa. Je, mtu akikosa chakula
akipendacho hawezi kula chochote ili kuuwa makali ya njaa? Hiyo
hufanyika sana………..!
No comments:
Post a Comment