Sunday, 2 March 2014

MDALASINI, TANGO NA ASALI....

  
jamani wenzangu nina jambo mlikuwa mnajua kama mdalasini, asali na tango ni dawa ya kumpa mtu nguvu kwenye mechi? kama ulikuwa hujui ndio ufahamu eti..



kuna dada mmoja alikuwa analalamika mpenzi wake nguvu kitandani hana, anasema jamaa akishatoa moja tu basi nguvu zote zinaisha jamaa hawezi hata kurudia ya pili, na hapo mwanamke wake huyo anakuwa hajatosheka lakini jamaa hajiwezi kabisa..




sasa huyu dada akawa anaomba ushauri kwa watu wazima akiwaeleza swala lake na mumewe watu wengi wakawa wanamshauri mengi tu pamoja na ya kwamba mumewe anywe maji ya mchele yale ya kwanza, sijui mwengine akamwambia anywe maji ya madafu kwa wingi na wengine wakimwambia aende kutafuta dawa za miti shamba...



akafika kwa bibi mmoja wa zamani (umri umeenda) yule bibi akamwambia yule dada ampe mumewe mdalasini pamoja na asali achanganye kwa pamoja atie na maji ama aiweke kwenye chai, halafu kila chakula cha yule baba kisikose kipande cha tango..



yule dada akafanya kama alivyoambiwa na yule bibi, sasa hivi dada anafuraha mambo si shwari, kwahiyo huu ni ushauri tu ya kwamba ukiona mwezio nguvu hana akienda moja anahema kama kasukuma trekta, mwanaume anahema kama presha imeshuka (hehehe) basi sio vibaya ukijaribu hayo..



lakini naomba niseme sio tu kwasababu huyu dada yeye mpenzi wake alipata nafuu ndio kila mtu itakuwa hivyo wengine vyao vya kurithi utalisha hivyo vitu milele jamaa hata kubadilika asibadilike...

No comments:

Post a Comment