Friday 26 April 2013

SIDIRIA SI SALAMA,Zasababisha maumivu ya mgongo, kuhema, moyo, zalegeza misuli......


SIDIRIA

Mtu anapovaa kwa muda mrefu lazima atapata fangasi kwa sababu ya jasho, lakini pia, hatakuwa huru anatakiwa auache mwili upate hewa” anasema


Kwa miaka mingi wanawake wamefunzwa kuvaa sidiria ili waweze kunyanyua maziwa yao au kuyaweka katika umbile la kupendeza.
Hata hivyo, sidiria imetajwa kuwa chanzo cha maradhi ya mgongo, misuli ya kifua, maradhi ya moyo na kusababisha kwa kiasi kikubwa  ugonjwa wa fangasi chini ya matiti, inapovaliwa kwa muda mrefu.
Utafiti mpya uliofanywa na wataalamu wa afya kutoka Chuo Kikuu cha Tiba cha Besancon, Ufaransa umebaini kuwa sidiria haimsaidii mwanamke zaidi ya kumsababishia maradhi kadhaa.
Profesa Jean-Denis Rouillon ambaye ametumia miaka 15 kufanya utafiti kwa wanawake  330 alibaini kuwa sidiria zina madhara kadhaa kwa wanawake akipingana na dhana iliyojengeka kuwa sidiria ni miongoni mwa mavazi muhimu kwa kundi hilo.
Profesa Rouillon hajawakataza wanawake kuvaa sidiria bali anasisitiza kutovaa kwa muda mrefu (mfano kulala nazo) na kutovaa mapema hata kama hunyonyeshi.
Sidiria haimpi manufaa yoyote mwanamke” anasisitiza Profesa Rouillon, ambaye katika utafiti wake alibaini kuwa wanawake ambao hawavai sidiria tangu usichana, wana maziwa imara yaliyozungukwa na misuli kakamavu kuliko wanaopendelea kuvaa nguo hiyo ya ndani.
Anasema kwa kiasi kikubwa binti anayeanza kuota maziwa anapovaa sidiria husababisha maziwa kuanguka mapema kuliko binti ambaye hatavaa sidiria.
Profesa huyo ambaye alianza kufanya utafiti tangu mwaka 1997 anasema alitumia rula na vifaa vingine kufanya utafiti huo na aligundua kuwa kuna tofauti ya milimita saba za urefu na msimamo wa maziwa kwa wasiovaa sidiria.
“Sidiria imekuwa kama tegemeo pale tu mwanamke anapoanza kuota maziwa, ina maana kwamba misuli inayobeba maziwa haitumiki na badala yake sidiria inachukua wajibu huo na hivyo misuli hiyo husinyaa kwa kukosa kazi” anasema
Anasema si kweli kuwa mwanamke asiyevaa sidiria maziwa yake huanguka bali huwa na ngozi nzuri zaidi katika viungo hivyo, huwa huru na matiti huwa katika umbile zuri zaidi.
Katika ushauri wake wa majumuisho ya utafiti huo Profesa huyo alisema: “Ni dhana potofu kudhani kuwa sidiria ni msaada kwa wanawake, ninachowashauri wanawake ni kutotegemea zaidi sidiria.”
Utafiti mwingine kama huu ulifanyika  Aprili 2012, nchini Uingereza  na Dk Nicholas Ericson  ambaye alibaini kuwa wanawake wanaovaa saizi kubwa ya sidiria wapo hatarini kupata saratani ya maziwa.
Gazeti la ‘Bussiness Week’ la nchini Marekani liliwahi kuandika ripoti kuwa viwanda vinavyotengeneza sidiria nchini humo vinapata mapato ya zaidi ya dola bilioni 11 (sawa na trilioni 17 na bilioni 600 Tsh)
Hata hivyo tafiti nyingine ziliwahi kufanyika na kugundua kuwa wanawake wasiovaa sidiria wakati wa mazoezi wamo hatarini kuharibu matiti yao.
Cletus Kiwale, Daktari Bingwa wa magonjwa ya wanawake anasema hajawahi kusikia iwapo sidiria ina madhara kwa mwanamke.
“Sidhani, labda sidiria inayobana sana, hata hivyo suala hilo linahitaji uchunguzi wa kina” anasema Dk Kiwale.
Naye Dk Sebalda Leshabari, Mwalimu wa Ukunga katika Chuo Kikuu cha Muhimbili anasema hakuna ukweli kuwa sidiria inasababisha madhara ila tu kwa wale watakaozivaa muda mrefu.

No comments:

Post a Comment