Kikosi cha Ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Dar Young African Spot Club 2013.
KLABU ya Coast Union ya Tanga imeipa Yanga ubingwa wa Ligi Kuu Bara baada ya kutoka sare ya bao 1-1 na Azam katika Uwanja wa Mkwakwani Mjini Tanga.
Bao la Azam ilifungwa na Agrey Morris katika dakika ya 57 kwa njia ya penalti huku bao la kusawazisha la Coast Union ikifungwa na Danny Lyanga katika dakika 71.
Kwa matokeo hao Yanga imetawazwa kuwa mabingwa wapya kabla ya pazia ya Ligi Kuu kufungwa, baada ya kukusanya pointi 56 mpaka hivi sasa huku ikiwa na mechi mbili mkononi.
Endapo Azam ingeshinda leo Yanga ingetakiwa kupata sare tu katika mechi yake na Coast itakayochezwa katika Uwanjawa Taifa jijini Dar es Salaam, kwani Azam iliyokuwa na pointi 48 ingefikisha pointi 51 na kubakiwa na mechi mbili mkononi.
Azam sasa ina pointi 49 hivyo hata ikishinda mechi zote mbili itafikisha pointi 55 wakati Yanga tayari inapointi 56 ambazo haziwezi kufikiwa na timu yoyote hata kama itafungwa katika mechi mbili ambazo ni kati wagosi wa kaya Coast Union na watani wao wa jadi Simba, ambayo imesha poteza mwelekeo katika mbio za ubingwa.
No comments:
Post a Comment