Friday, 14 June 2013

Marekani imefuta safari ya Obama kuja Tanzania


Rais wa Marekani Barack Obama na Mkewe Michelle Obama,wakiwapungia wafuasi wao baada ya kuhutubia wakati kampeni za nchi hiyo.
WAKATI Serikali ya Tanzania ikiendelea na maandalizi yaRais waTanzania akitafakari jambo kupokea msafara wa watu 700 waliotarajia kuingia nchini kwa ziara ya Rais wa Marekani Barack Obama, Rais huyo amesitisha safari yake.
Ikulu ya Marekani imetangaza kwamba msafara wa Rais Obama kuja kutembelea Bara la Afrika haitakuwepo tena,baada ya serikali ya nchi hiyo kukosa fedha itakayoweza kugaramia safari ya Rais huyo.
Taarifa iliyonaswa na Waandishi  kutoka katika mitandao mbalimnali  nchini Uingereza na Marekani  zinaeleza kwamba mbali na suala la bajeti ya Rais huyo kuja nchini Tanzania kuwa kubwa pia kamati ya sheria ,ulinzi na usalama wa Marekani imeshindwa kuthibitisha juu ya suala la ulinzi na Usalama wa Rais Obama katika kipindi chote atakachokuwa nchini Tanzania pamoja na baadhi ya nchi Barani Afrika.
Taarifa hiyo pia ilieleza kwamba msafara wa Rais Obama unahitaji maandalizi ya kutosha kwa sababu ni msafara unaohusisha watu wengi pamoja na vyombo mbalimbali vya ulinzi ikiwemo wanyama.
Msemaji wa Ikulu ya Marekani alisema kwamba serikali ilijaribu kuangalia uwezekano wa Rais Obama kuja Tanzania na baadaye kutembelea Senegel pamoja na Afrika Kusini ambapo alitakiwa kukaa Tanzania kwa saa mbili tu lakini gharama za ulinzi imekuwa kubwa sana.
Rais wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete, (kulia) akisalimiana na Rais wa Marekani Barack Obama,alipomtembelea rais huyo Ikulu ya Marekani"Katika msafara wa Obama inatakiwa kuwe na ndege mbili za mwendo kasi, kwa ajili ya kulinda ndege ya Rais,iwepo ndege za askari wa majini zinazotembea kwenye meli habarini, iwepo pea maalum za magari zitakazo sushwa katika nchi zote tatu mapema kwa kutumia ndege za jeshi kwa ajili kuimarisha ulinzi kabla ya Rais kutua katika nchi hizo" alisema Mseaji wa Ikulu ya marekani Josh Earnest.
Nakala ya taarifa hiyo iliyonaswa na Waandishi  pia ilimkariri msemaji huyo wa Ikulu ya Marekani akisema kwamba pia katika msafari huo ni lazima iwe na vifaa maalum vya kutolea matibabu katika kipindi chote cha ziara ya Rais, lazima pia iwe na chombo maalum kwa ajili ya waandishi mbalimbali wa habari pamoja na vyombo vingine vya usalama kwa ajili ya kutoa taarifa ya safari ya Rais ,pamoja ndege zitakazokuwa zikizunguka kuangalia hali ya usalama katika hoteli zote atakapo kuwa ana alala Rais Obama na msafara wake.
Taarifa hiyo ilifafanua kwamba safari hiyo ndiyo safari kubwa kuliko aliyowahi kuifanya Barani Afrika ambapo alifika nchini Ghana, tangu alipochaguliwa kuwa Rais wa Marekani mwaka 2009 ambapo inakadiriwa kuwa itachukua kati ya dola za marekani 60 million sawa na tsh bilioni 96,000,000,000 na dola 100 milion sawa tsh bilioni 160,000,000,000.

 

No comments:

Post a Comment