Friday, 14 June 2013
Rais Museveni amkoromea Rais wa Misri
RAIS wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni ameionya serikali ya Misri na kuitaka iache mara moja mpango wake wa kutaka kuzuia nchi zinazozunguka Mto Nile kuacha kutumia maji ya mto huo.
Musen alisema hayo wakati alipokuwa akizungumzia Bajeti ya Serikali iliyosomwa jana Bungeni, Museveni alimtaka Rais mpya wa Misri Muhammad Morsi. kufuta mikakati yake ya kuzuia matumizi ya maji ya Mto huo.
“ Niliona taarifa ya Serikali ya Misri katika vyombo vya Habari ikiitaka Serikali ya Ethiopia kusitisha matumizi ya maji ya Mto Nile, Ethiopia inafanya jambo ambalo nchi yoyote Barani Afrika ingependa kukifanya"alisema Rais Museven na kuongeza.
"Mradi wa nishati ya umeme uliojengwa na Ethiopia katika Mto huo ni jambo la msingi na la kupongezwa, Afrika haiwezi kuiumiza Misri na wala Misri haiwezi kuimuza Mwafrika mwenye ngozi nyeusi tena".
Akizungumza na wabunge wa nchi hiyo pamoja na wanadiplomasia waliohudhuria mkutano huo katika Hoteli ya Serena, Museveni alisema kwamba maji ya Mto Nile ni mali ya nchi zote zinazopakana na Mto huo.
Awali Rais wa Misri Muhammad Moris aliema kwamba, "Mimi kama rais wa taifa la Misri ninawakikishia kwamba njia zote zimefungulia, maisha ya wamisri yameunganishwa sehemu zote kama watu wenye nguvu na damu zetu ni kitukimoja,hivyo hatuwezi kuruhusu mtu yeyote acheze mali zetu pamoja na maji yetu".
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment