
Mgombea Urais wa Democratic Progressive Party (DPP) nchini Malawi, Peter Mutharika, amesema hakuna sababu za kufanya majadiliano kuhusu Ziwa Malawi ambalo Tanzania wanaliita Ziwa Nyasa.
 Mutharika, ambaye ni mwanasheria, aliyasema hayo kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika juzi  Mkoa wa Kati.
                
              
Akikaririwa na gazeti la  Nyasa Times, Mutharika  alisema Tanzania haina cha kuambulia kwa Ziwa Malawi.
Kiongozi huyo ambaye hakuwapo katika mkutano wa 
Rais Joyce Banda na wapinzani kuzungumzia mustakabali wa ziwa, 
aliwahakikishia Wamalawi kuwa wasiwe na wasiwasi wa mvutano huo.
  
Mutharika ziwa lote ni mali ya Malawi na  akisisitiza kuwa, Tanzania haina hata punje ya eneo.
 “Hakuhitajiki majadiliano, Ziwa Malawi ni mali ya
 Malawi, litakuwa la Malawi,” alisema Mutharika ambaye alichukua masomo 
ya Sheria Tanzania.
                
              
 “Tanzania inatumia nafasi ya udhaifu wa uongozi 
wetu, lakini ukweli, hawana hata tone la eneo... Tutakapoitwa kwenye 
uchaguzi ujao mwakani, tutamaliza haya yote. 
"Nitaleta meli nyingi kwa 
ajili ya maendeleo ya uchumi, kutengeneza ajira za kutosha kwa vijana,” 
alisema Mutharika huku akishangiliwa na wafuasi wake.
  
                
              
Tanzania inataka kugawana ziwa, lakini Malawi 
imegomea mpango huo na suala hilo liko katika majadiliano ambayo Banda 
alisema kama mwafaka haukupatikana ifikapo Septemba 30, Malawi itapeleka
 suala hilo Mahakama ya Kimataifa (ICJ).
 
 
 
No comments:
Post a Comment