Assalam Alaikum! Ni
furaha yangu kwa mara nyingine tena kukutana nanyi wapendwa wasomaji wa
safu yetu hii ya uwanja wa mapenzi. Tumshukuru Muumba wetu kwa
kutujaalia uhai na afya njema, lakini zaidi ya hapo tumshukuru pia kwa
kutuumbia kitu mapenzi au sio?
Siku zote hatutaacha kuzungumza juu ya mapenzi kwani ni ukweli usiopingika kwamba mapenzi ndio maisha yetu. Tunafanya
kazi usiku na mchana, tunahangaika huku na huko, lakini mwisho wa siku
tunafikiria jinsi gani tutapata kuboresha na kufurahia maisha na wapenzi
wetu. Tunafikiria pia ni jinsi gani tunaweza tukapata utulivu na amani
katika maisha ya kimapenzi na wapenzi wetu, waume zetu au wake zetu
katika siku zote za maisha yetu.
Wiki hii nimeona ni vyema tukabadilishana uzoefu juu ya suala zima la wivu katika mapenzi. Mtakubaliana
nami kuwa suala la kuwa na wivu kwa mpenzi wako ni jambo lisilokwepeka
hasa kwa sababu kubwa ya kuaminika kwake kwamba kuwa na wivu ni moja ya
kigezo cha kuonesha ni jinsi gani unampenda mpenzio na kwamba hauko
tayari kwa namna yoyote ile kushea na mwingine ndio maana wanawake wengi
hawataki kusikia suala la ukewenza kabisaa! Hata kama jambo hilo
limepewa baraka zote na dini au tamaduni zao.
Lakini
kubwa katika wivu ni ile kutokuwa tayari kuona tunasalitiwa na wapenzi
na hasa kwa wale tunaowapenda ukweli toka moyoni mwetu na zaidi ukute
ndo tumeshawagharamikia kiasi cha kutosha na kujitoa kwao kwa kila kitu!
Umeshawahi
kusikia kauli kama “Jamani mke (au mume) anauma! Au kauli kama mke wa
mtu sumu” na hugeuka sumu kweli hasa pale “unapobambwa” na mali za
wenyewe, kufanyiwa “kitu mbaya” inakuwa sio jambo la ajabu sana.
Niwaambie
kitu wapenzi wasomaji! Mapenzi bwana ni “full uchoyo, ni full
kujipendelea! Mpenzi wanaume kwa mfano, anaweza kufikiria kwamba ni yeye
tu ndiye anayestahili na anayeweza kumfanya mpenzi wake acheke na
kufurahi.
Na
kwamba akitokea mwanaume mwingine akapata nafasi ya kumfurahisha mpenzi
huyo hata katika stori za kawaida tu, unaweza ukasikia akisema, “Hivi
wewe mna nini na huyo jamaa, mbona unamchekea chekea hivyo, au…!” Hiyo
ndiyo choyo ya penzi, na kikubwa kinachofanyika hapo ni ile tu kujaribu
kulinda maslahi binafsi.
Pamoja
na ukweli kwamba tabia ya wivu inapozidi hugeuka kuwa kero, lakini
kabla hatujafika huko hebu tuangalie nafasi ya wivu katika mapenzi yetu. Yaani swali ni kwamba, je! Wivu katika mapenzi unaleta maana?
Nionavyo mimi wivu ukitumika vizuri unaleta maana na una nafasi muhimu sana katika mapenzi kwa sababu zifuatazo:
Huonesha kujali
Sote
tunaamini pasipo na wivu hata chembe, hapana mapenzi ya kweli.
Kumuonesha wivu mpenzi wako ni kumjulisha ni kiasi gani unamjali na
kumpenda na kwamba yeye ni mtu maalum sana kwako.
Jamani,
mahali penye mapenzi yasiyo na wivu hata kidogo, panatia shaka! Na mara
nyingi majibu yake ni kutokuwa “sirias” katika uhusiano huo au huenda
kuna kupitisha muda tu na kwamba labda hakuna “future” na mpenzi huyo au
ni dalili ya kuchuja kwa penzi.
Kuthamini uhusiano
“Sio
kama sikuamini dear, bali wivu wangu kwako ni katika kuuthamini
uhusiano wetu, mimi na wewe ni umoja wenye thamani kubwa, tusiruhusu
kuuchezea nje yetu! Huu ni mfano wa ujumbe unaoonesha maana na nafasi ya wivu katika mahusiano ya kimapenzi.
Kukumbushana
Kauli
au matendo yanayoashiria kumuonesha wivu mpenzio yanasaidia kwa kiasi
kikubwa kumfanya mwenzi wako “asijisahau” katika jukumu la kulienzi
penzi lenu hata akiwa mbali ya upeo wa macho yako.
Kujijengea heshima
Kwa namna moja au nyingine, wivu pia huweza kukujengea heshima. Kwa
mfano mume mwenye wivu na mkewe hujijengea heshima ya kwamba kweli
anamjali na kumpenda mkewe lakini pia anaweka mazingira ya kutosumbuliwa
kwa mke wake huyo kumjengea heshima yake kama mke wa mtu.
Husaidia kubadilisha tabia
Ukiwa
na wivu, unaotokana na mavazi “tatanishi” anayopendelea kuvaa mpenzi
wako kwa mfano, huenda ikasaidia kubadili tabia yake.
No comments:
Post a Comment