Mavazi hukinga mwili dhidi ya baridi au jua kali na athari nyingine zinazoweza kuathiri mwili vibaya
Kazi
nyingine ya mavazi ni kuwasilisha ujumbe kwa watu wengine kwa kuonyesha
mtu fulani ni sehemu ya kundi fulani kama vile watoa huduma kwa jamii
kama manesi, askari, wachungaji n.k.
Mavazi
kwa hakika ni kiashiria cha nje kinachoakisi na kuonyesha taswira ya
kile kilichoko ndani ya mtu. Muonekano wa mtu wa nje unatoa picha ya ule
wa ndani.
Kumekuwa
na tatizo kubwa la wanawake wengi Tanzania na Afrika kwa ujumla kuvaa
mavazi yanayoonekana kwa wengi kama ya nusu uchi, yanayobana sana kiasi
cha kuchora viungo vyote vya miili ya wavaaji na yale yanayoitwa vimini.
Mavazi
nayo yamekuwa kichocheo kikubwa cha watu kutumbukia kwenye vitendo vya
ngono, uzinzi, uasherati na kusalitiana kiasi cha kusababisha watu wengi
kushindwa kuzuia tamaa za mwili kulingana na kiwango cha ustahimilivu
alichonacho mtu.
Nguo fupi na zile zilizobana zimewafanya baadhi ya wanaume kushindwa kujizuia hivyo kuanguka katika matamanio.
Wanawake
wameumbwa kwa maumbile tofauti, lakini katika suala la uvaaji, wengi
hawajali ni kwa kiasi gani watazua mfadhaiko kwa wanaume.
Hili linadhihirishwa na mwalimu
Frank
Molel anayesema: “Kuna maumbile ya mwanamke ambayo mwanaume hatakiwi
kuyaona kwa macho ndio maana mabinti wanatakiwa kujisitiri kwa kuvaa
mavazi ya heshima. Wanawake wameumbwa kwa umbo zuri ili wawafunulie
waume zao uzuri wao na si kuutembeza barabarani.”
Mwalimu
Frank anasema kuwa wanawake na mabinti wengi sasa wanavaa nguo
zinazoacha sehemu kubwa ya mapaja yakiwa wazi, hali ambayo tofauti na
Wazungu huwavutia wanaume na kujawa na tamaa.
Sasa sio
jambo la siri kwa wanawake na wasichana wengi kuvaa nguo zinazobana
kiasi cha kuchora umbile zima la mwanamke, kitovu wazi.
Mwalimu
huyo anasema baadhi ya wanawake na wasichana wanaojua kuwa wamejaliwa
maumbile mazuri, huvaa mavazi sio kwa nia ya kujisetili bali kuwavutia
wanaume ili washawishike kuingia kwenye vitendo vya ngono na kisha
kulaumu kuwa ni tamaa za wanaume bila kujua kuwa chanzo ni wao.
Wako
wanawake wanaojidanganya kuwa kuvaa nusu uchi, vimini na nguo za kubana
zinazochora miili yao ndio kupendeza jambo ambalo si kweli kiuhalisia wa
mambo, kimaadili ya Kitanzania na Kiafrika na hata kinyume na maagizo
ya dini.
Utafiti
unaonyesha kuwa wanaume wengi wanaopenda kuwaona wanawake na wasichana
wakiwa wamevalia vimini na nguo za kubana sio waoaji, bali wanapendelea
sana mfumo huu wa mavazi ambao unawasaidia kuchagua yupi wa kumtumia.
Kuna sehemu za maungo ya mawanamke ambazo mwanaume hatakiwi kuziona lakini sasa zimefanywa kuwa za kawaida.
Itakumbukwa kuwa miaka ya nyuma nguo fupi zilipigwa marufuku na baadhi ya wanawake walikamatwa na kufunguliwa mashtaka.
Zipo
baadhi ya familia ambazo mama na binti zake wote huvaa vimini. Hakuna wa
kumkosoa mwenzake na kumrekebisha. Ukiuliza unaambiwa ‘tunakwenda na
wakati’.
Uvaaji
wa aina hii umeshazua balaa sehemu kadhaa hapa nchini. Itakumbukwa kuwa
katika jiji la Dar es Salaam, kilizuka kikundi cha vijana ambao walikuwa
wakiwakamata wasichana na wanawake wanaovaa nguo fupi na kuacha sehemu
kubwa ya miili yao wazi, na kuwachania nguo.
Baadhi ya mikoa, vijana hawa wamekuwa wakiwakamata wasichana na kuwabaka.
Katika
jiji la Arusha maeneo ya Metropole , vijana waliomshuhudia binti mmoja
mrefu aliyekuwa amevalia nguo fupi sana kiasi cha kukaribia kuonekana
kwa nguo ya ndani walisikika wakipiga kelele na kumzomea binti huyo huku
wengine wakilalamikia hali ile.
“Hivi ni kweli baadhi ya wanawake hawajui thamani yao kiasi cha kuacha maungo yao wazi na kutojisitiri kama inavyotakiwa.”
Je, ni kweli kwamba binti au mama hawezi kupendeza akivaa nguo nzuri zisizobana wala kuacha wazi sehemu kubwa ya mwili wake?
Je, msichana au mwanamke hawezi kuvutia na hivyo kupata mwenzi akiwa kavaa mavazi ya heshima yanayositiri mwili wake?
Je, msichana au mwanamke hawezi kuendelea hadi tu avae ‘vijinguo’ vinavyotakiwa kuvaliwa na mdogo wake au mwanae?
Ni kweli kwamba kila mtindo wa mavazi unaoingia nchini kutoka kwa weupe unafaa kwa wanawake na mabinti wa Afrika?
Kila
mtindo wa uvaaji wa nguo sharti ulinde thamani, heshima na hadhi ya
mwili wa mwanamke, na sio kuwa kichocheo cha matamanio ya ngono.
“Hata kama heshima ni bure wasipojiheshimu hatutawaheshimu.”
Ni kauli
ya mwandishi wa vitabu na makala mashuhuri Richard Mabala katika makala
yake inayoelezea umuhimu wa mtu kujiheshimu yeye mwenyewe ndipo
astahili kuheshimiwa na wengine.
Maadili yanavyozidi kuporomoka kila siku nani alaumiwe? Wazazi, walezi, watoto, jamii au serikali?
Serikali
inapaswa kutunga sheria na sera za kulinda utamaduni wetu wa Kitanzania
na Kiafrika ili usiathiriwe na utandawazi ambao tusipoangalia utauzika
utamaduni wa Kiafrika endapo tutaacha kuulinda na kuudumisha
No comments:
Post a Comment