Faida hii haina pingamizi kwa sababu ya ukweli kwamba watu wanaokuwa katika mahusiano ya karibu wanajijengea hisia na nguvu fulani ambayo huwasaidia kusaidiana na kujaliana wakati wa shida. Siyo tu kwamba watu walioko katika mahusiano ya aina hii wanaishi muda mrefu lakini pia ni kweli kwamba wanakuwa na furaha na wanaridhika na maisha kuliko wale wanaoshindwa kukaa katika mahusiano.
· Pili, kuwa katika mahusiano mazuri ya mapenzi kunasaidia katika mambo
mbalimbali ya kimahitaji. Kusaidiana katika mahitaji mbalimbali baina ya
wapenzi ni njia nzuri ya kuwa na maendeleo. Watu wawili wanaoshirikiana
pamoja mara nyingi watakuwa na maisha mazuri zaidi ya yule anayefanya
peke yake. Unapokuwa na mtu karibu wa kusaidiana naye katika mahitaji ni rahisi kupata mafanikio.
· Tatu,
Watu walio katika mahusiano mazuri wanapata msaada wa kijamii; kwa
maana ya kuwa na mtu karibu ambaye anajali mahitaji yako ya msingi na
hisia zako. Kuwa na msaada wa aina hii kuna faida nyingi, mojawapo
muhimu ni kuweza kufanya maamuzi ya busara bila kuwa na mtindio wa
mawazo na hofu ama mashaka.
· Nne, kuwa na mwenza katika maisha hufanya maisha kuwa ya faraja zaidi.
Kuwa na mtu ambaye mnaweza kushirikiana mambo madogo madogo ya maisha kama
kuangalia Tv, kutembea, kula pamoja ni muhimu; inaboresha mahusiano na
mara nyingi watu walio katika mahusiano ya aina hii wamekuwa na maisha
bora zaidi.
· Tano, Mahusiano ni muhimu kwa sababu wapenzi wana kawaida ya
kuangaliana tabia zao hasa zile ambazo ni haribifu, na wamekuwa na
kawaida ya kuonyana ama kushauriana kuacha kufanya mambo mabaya na tabia
mbaya. Kwa mfano watu walio katika mahusiano ya karibu wamekuwa na
tabia ya kujaribu kuwashauri wapenzi wao kuacha kuvuta sigara, kupunguza
pombe, kuacha kutumia madawa ya kulevya nk.
· Mwisho, Watu walio katika mahusiano bora ya kimapenzi wanafanya
mapenzi mara nyingi zaidi kuliko wale walio pekee. Kufanya mapenzi mara
kwa mara, kimpangilio ni muhimu kwa afya bora ya mwili na akili. *Ni
muhimu kuzingatia kwamba kufanya huko mapenzi ambako ni bora kwa afya ya
mwili siyo kubadilisha wanaume ama wanawake, ila ni kwa mwenza wako ama
mke au mume na katika hali ya maelewano, uhuru na amani lakini pia kwa
utaratibu unaostahili ndiyo upelekea kuleta faida hiyo.
Baada ya kusema yote hayo, ni ukweli kwamba mahusiano mazuri baina ya
wapenzi huwa na faida nyingi kwa watu wenye bahati ya kupata mtu wa
kumpenda na hatimaye nao kupendwa pia.
No comments:
Post a Comment