Wanajeshi wa Marekani nchini Afghanistan wamemipiga risasi
kimakosa mtoto mmoja wa miaka minne na kuzidisha uhusiano
mbaya unaotokota kati ya nchi hizo mbili. Uhusiano kati ya Marekani
na Afghanistan
umezorota zaidi kufuatia kukataa kwa Rais Hamid
Karzai kutia saini makubaliano ya pamoja ya kiusalama
yatakayoruhusu majeshi ya Marekani kusalia nchini mwake hata
baada ya majeshi ya kigeni kuondoka mwaka huu.
Marekani
imesema jeshi lake haliwezi kusalia Afghanistan bila ya makubaliano
hayo.Karzai anaitaka Marekani kusitisha operesheni zake zote za
kijeshi nchini humo miongoni mwa masuala mengine kabla ya kutiwa
saini kwa makubaliano ya kiusalama kwani anahoji inasababisha vifo
vya raia wake.
Msemaji wa jimbo la Helmand amesema wanajeshi
hao walimuua kijana huyo wakidhani ni adui.Msemaji wa jumuiya ya
kujihami ya NATO amesema wanachunguza kisa hicho na kwamba
kila hatua zitachukuliwa kuepusha vifo vya raia.
No comments:
Post a Comment