Rais wa Ufaransa Francois Hollande anapanga kulichukulia hatua za
kisheria jarida moja nchini humo,kwa kuingilia maisha yake ya
kibinafsi baada ya jarida hilo la Closer kudai kuwa ana uhusiano wa
kimapenzi na muigizaji sinema mmoja wa kike.
Taarifa zinasema
Hollande anazingatia kulichukulia hatua jarida hilo kutokana na
kuingiliwa maisha yake ya kibinafsi ambayo ni ukiukaji wa haki zake
kama raia wa Ufaransa. Jarida hilo linalochapishwa kila wiki,
lilichapisha picha saba zinazoonyesha mwanamume anayedaiwa
kuwa rais huyo wa Ufaransa akitoka kwenye jengo moja la makaazi
akiandamana na mlinzi wake na picha za mwanamke huyo muigizaji
anayedaiwa pia akiingia na kutoka jengo hilo hilo.
No comments:
Post a Comment