KLABU ya Manchester United inahofia Robin van Persie anaweza kuendelea kuwa nje kwa wiki sita zaidi baada ya kuumia paja sehemu ile ile aliyowahi kuumia alipokuwa Arsenal.
David Moyes anayemuhitaji sana mshambuliaji huyo wake hatari arejee uwanjani kutokana mwenendo mbaya wa timu hivi sasa, jana Ijumaa amethibitisha kwamba Wayne Rooney pia anaweza kukosa mechi ya leo dhidi ya Swansea.
Lakini mtu anayemuumiza kichwa aswa Moyes ni Van Persie, kocha huyo amesema kwamba hawezi kutaja tarehe ya kurejea uwanjani kwa mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 30, hata baada ya kumpeleka Uholanzi akafanyiwe kazi na kocha wa viungo wa PSV Eindhoven.
Hasara juu ya hasara: Van Persie anaweza kuwa nje kwa wiki sita zaidi baada ya kuumia paja
Kuna wasiwasi Van Persie akawa nje kwa muda mrefu zaidi, kwa sababu ameumia sehemu ile ile ambayo aliwahi kuumia akiwa Arsenal Desemba mwaka 2007 na akakaa nje kati ya Desemba 16 na Machi 9, akicheza mechi 15 tu.
Mholanzi huyo hajakitumikia kikosi cha Moyes tangu Desemba 10 na jana kocha wa United amesema pia kwamba Rooney amepelekwa Misri kwa matibabu sababu ya hali ya hewa pamoja na maofisa wa dawati la tiba la timu hiyo, ili aweze kuwahi mechi na Chelsea
No comments:
Post a Comment