Madrid, Hispania. Lionel Messi amefunga mabao
mawili akiwa amerejea baada ya kukaa nje kwa miezi miwili akisumbuliwa
na tatizo la misuli na kuisaidia Barcelona kuichapa Getafe 4-0 katika
mchezo wa kwanza wa raundi ya tano ya Kombe la Mfalme.
Tangu alipoumia Novemba 10 mwaka jana, Messi
aliingia uwanjani kwa mara ya kwanza kuchukua nafasi ya Andres Iniesta
alifunga bao lake la kwanza dakika ya 61 na ya 87 akimalizia kazi ya
Martin Montoya. Hilo lilikuwa ni bao lake la 16 na 17 msimu huu.
‘’Nilijisikia vizuri wakati wa mazoezi pamoja na
kuwa walinifanyia vipimo lakini unapoingia uwanjani kila kitu kinakuwa
tofauti,’’ alisema Messi na kuongeza. ‘’Mwili wangu upo safi kabisa,
sijahisi maumivu yoyote ya misuli.’’
‘’Nilicheza nikiwa ni majeruhi,’’ alisema Messi ambaye alikuwa nje ya uwanja kwa siku 59.
‘’Lakini nashukuru nimefanikiwa nimepona na sasa nimeanza vizuri mwaka huu.’’
Mwanasoka huyo bora mara nne wa Fifa alikosa mechi 12 za msimu huu kwa sababu ya kuumia.
Cesc Fabregas aliifungia Barcelona bao la kuongoza
dakika ya saba na kupachika la pili kwa mkwaju wa penalti 61, likiwa
ni bao lake la 11.
Mechi ya marudiano dhidi ya Getafe itafanyika Januari 16.
Real Betis inayoshika nafasi ya mwisho katika Ligi
ya Hispania, iliichapa Athletic Bilbao, nayo timu ya daraja la pili ya
Alcorcon ilishinda 1-0 dhidi ya Espanyol huku Racing Santander wakitoka
sare na Almeria.
Manchester City iliisambaratisha West Ham 6-0
katika mchezo wa kwanza wa nusu fainali ya Kombe la Ligi, huku Alvaro
Negredo akifunga mabao matatu.
Hicho ni kipigo cha pili kikubwa kwa West Ham ndani ya siku nne.
Edin Dzeko alifunga mabao mawili na Yaya Toure
moja kwa City, inayosaka kucheza fainali ya Kombe la Ligi kwa mara ya
kwanza tangu walipofanya hivyo mwaka 1976.
No comments:
Post a Comment