Wanawake
wa Kenya wanaofanya biashara ya kuuza Samaki katika ufuo wa ziwa
Victoria mjini Kisumu Magharibi mwa nchi, wanajaribu kukomesha tabia ya
kujihusisha na wavuvi kingono ili wapewe Samaki bila malipo.Tabia hii
imelaumiwa pakubwa kwa kuchochea ongzeko la maambukizi ya HIV.
Wakati
wanawake hao wanapokubali kuwa na uhusiano wa kingono na wavuvi
wanaume, basi hilo huwa kama hakikisho la kupata Samaki wa kuuza kwa
kipindi kirefu.
Biashara
hii inayojulikana na wenyeji kama Jaboya, ambapo mwanamke anafanya
Ngono na wavuvi ili apate Samaki wa kuuza, imelaumiwa pakubwa kwa
kueneza maradhi ya Ukimwi miongoni mwa watu wanaoishi katika maeneo ya
Ziwa Victoria.
Sasa wanawake katika eneo hilo wamezindua kampeni inayolenga kukomesha biashara hiyo.
Mradi
uliozinduliwa na taasisi ya utafiti wa mazingira ya Victoria, imeanza
kuwapa wanawake hao maboti yao ili waweze kufanya uvuvi wenyewe.
Dan
Abuto, afisaa mmoja wa shirika hilo, anasema kuwa pesa watakazolipa
wanawake hao kutokana na biashara zao za Samakai, zitawaruhusu kutengeza
boti zao wenyewe.
"mradi huu unalenga kushughulikia 'Jaboya'
kama swala la afya ya umma , kupunguza viwango vya umasikini na kuleta
usawa wa kijinsia,'' alisema afisaa huyo.
Wajane pia wanasemekana kuwa katika hatari kubwa zaidi kutokana na biashara hiyo hasa ikiwa ni jukumu lao kulisha familia zao.
Makundi
ya wanawake yanasema kuwa boti hizo za thamani ya dola 920,
hazitamaliza tu biashara hiyo bali pia itapunguza kuenea kwa maradhi ya
Ukimwi. Ikiwa mradi huu utafanikiwa basi maambikizi nayo yatapungua
pakubwa.
No comments:
Post a Comment