Wananchi wa Kenya wameshangazwa na taarifa ya mwanamume mmoja
aliyedhaniwa kuwa mfu kufufuka kutoka katika chumba cha kuhifadhia maiti katika
hospitali moja mjini Naivasha umbali wa kilomita tisini kutoka mji mkuu
N
airobi.
airobi.
Mwanamume huyo Paul Mburu mwenye umri wa miaka 24, alipelekwa hospitalini kwa
matibabu baada ya kunywa sumu kwa lengo la kujitoa uhai,kutokana na ugomvi wa
kinyumbani na babake ingawa alisemekana kufariki Jumatano usiku wakati akipokea
matibabu
Wafanyakazi wa hospitali hiyo walipigwa na butwaa na hata kutoroka walipoona
mwili wa mtu aliyedhaniwa kufariki ukisonga na kuonyesha dalili za kuwa hai
katika chumba cha kuhifadhia maiti.
Afisaa mkuu wa matibabu katika hospitali hiyo ya wilaya, Dokta Joseph Mburu,
alisema kuwa dawa iliyotumiwa kumtibu Mburu hufanya moyo kupiga polepole hali
ambayo huenda ilimfanya muuguzi kudhani kuwa mgonjwa alikua amefariki.
Mwanamume huyo alisikika akimtaka mmoja wa wafanyakazi katika chumba cha
kuhifadhia maiti kumsaidia kwani alikuwa anahisi baridi kali na hapo ndipo mmoja
wa wafanyakazi alipotimua mbio kwa hofu.
Nusura Mburu awekwe kwenye jokovu la kuhifadhia maiti.
Jamaa za mwanamume huyo akiwemo babake walikuwa wametembelea chumba cha maiti
siku ya Alhamisi ili kujiandaa kwa mazishi , lakini baadaye mchana
walifahamishwa kuwa Mburu alikuwa hai.
No comments:
Post a Comment