MSIGWA AFIKISHWA MAHAKAMANI KWA VURUGU
Mbunge
wa Iringa Mjini, Mch. Peter Msigwa amefikishwa katika mahakama ya
wilaya ya Iringa muda mfupi uliopita akidaiwa kuhusika na uchochezi na
kusababisha vurugu katika kampeni za udiwani Kata ya Nduli.
Mch. Msigwa alikamatwa jana jioni baada ya kutokea kwa vurugu hizo katika mkutano wa kampeni wa chama cha Chadema.
Baada ya kusomewa mashtaka yake amekana na ameachiwa huru kwa dhamana, kesi hiyo itatajwa tena Machi 10 mwaka huu
No comments:
Post a Comment