UNGEBAHATIKA kumuona mwanaume mmoja,
mkazi wa Sharif Shamba, Ilala jijini Dar, Beda Mloka ‘Baba Tony’
alivyokuwa ametapakaa damu chapachapa, lazima uulize kulikoni ambapo
jibu ni moja tu la kushangaza, kisa cha yote hayo ni fumanizi, Risasi
Mchanganyiko lina kisa cha kusikitisha.
Habari
kamili zilizonaswa na gazeti hili ni kwamba mwanaume aliyetajwa kwa
jina la Baba Asha alidai kumfumania rafiki yake wa karibu, Baba Tony
akiwa gesti na mkewe (jina linahifadhiwa), tayari kwa ‘kugagadua’ naye
amri ya sita.
Tukio hilo la aibu ya milenia
lilijiri katika nyumba ya kulala wageni ya Pumzika iliyopo maeneo ya
Msimbazi Center, jijini Dar ambapo mara baada ya kumtia mikononi ‘mwizi’
wake ambaye mbali na urafiki pia ni majirani, ndipo akamchakaza sura
vibaya na kumsababishia kuvuja damu chapachapa.
Habari za kina zilidai kuwa mke wa
Baba Asha alikuwa bafuni akioga, mara ukaingia ujumbe mfupi ‘sms’ kwenye
simu yake ya kiganjani, ndipo mumewe akachukua kilongalonga hicho na
kuufungua ujumbe huo.
Ilidaiwa kuwa mume alitaharuki kukutana na ujumbe uliokuwa ukimtaka mkewe kwenda Pumzika Guest House kukutana na jamaa huyo.
Iliendelea
kudaiwa kuwa Baba Asha hakuyaamini macho yake, akausoma tena ule ujumbe
na ndipo akagundua sms nyingine nyingi, vocha na fedha za mtandao
alizokuwa akitumiwa ‘mai waifu’ wake kutoka kwa Baba Tony.
Chanzo kilidadavua kuwa baada ya
kugundua mchezo mzima, Baba Asha akatulia na kumsubiri mkewe atoke
bafuni ili kuliweka sawa suala hilo.
MKE HUYO
Ilifahamika kuwa mke aliporudi kutoka
kuoga, mume hakuonesha dalili zozote, alichokifanya ni kumwita mkewe na
kumwambia kuwa achague moja, kufungasha kilicho chake, aondoke nyumbani
kwake au amwekee jamaa mtego anaswe ili ajue mke wa mtu ni sumu.
Jibu lilikuwa rahisi kwani alikubali kuweka mtego ili amnase mbaya wake ndipo atamsamehe.
ACHEZWA NA MACHALE
Ilifahamika kuwa ilipita wiki moja
kimyakimya kwani mara ya kwanza Baba Tony alichezwa na machale,
alipofika kwenye gesti hiyo na kumwona mtu anayemfahamu, alimwambia yule
mwanamke waahirishe.
Habari za uhakika ni kwamba wiki
iliyopita, Baba Tony aliingia kwenye kumi nane, akajaa mzimamzima kwenye
mtego wa fumanizi uliowekwa na Baba Asha na mkewe.
RISASI MCHANGANYIKO LATONYWA
Baada ya kupata uhakika kuwa kuna
tukio, ndipo chanzo chetu kikalitonya Risasi Mchanganyiko kuwahi eneo la
tukio na kuwa ‘stendibai’.
Chanzo: Risasi Mchanganyiko mna habari?
Risasi
Mchanganyiko: Habari tunazo nyingi na nyingine zipo kwenye uchunguzi,
si unajua Oparesheni Fichua Maovu ipo kazini? Lakini kama una ya kwako
tupe tuifanyie kazi mara moja.
Chanzo: Kwa taarifa yenu hapa Pumzika Guest House, Ilala kuna fumanizi, jamaa anamfumania rafiki yake na mkewe.
Risasi Mchanganyiko: Zungumza taratibu, tunashukuru kwa taarifa, tupe dakika sifuri.
‘NGOMA’ ILIKUWA HIVI
Kweli, ndani ya dakika sifuri, gazeti hili lilikuwa limejaa tele, tayari kwa fumanizi ambapo ‘ngoma’ ilikuwa hivi:
Mara baada ya kuona mwanaume mmoja
(Baba Asha) akiwa na askari kwenye gesti hiyo akihaha, king’ora kililia
kwenye akili ya paparazi wetu ambaye hakufanya makosa, akamfuata
mfumaniaji kwa nyuma hadi aliporuhusiwa kumfuata mkewe chumbani.
Chumbani mtiti ulikuwa mkubwa ambapo
Baba Tony alikutwa kama alivyozaliwa huku mke wa mtu akiwa bado hajavua
na ndipo mtiti ukaanza.
Katika purukushani, Baba Asha alimpa
kibano ‘mwizi’ wake hadi akamchana usoni na kumng’oa meno ya mbele,
jambo lililosababisha kutokwa na damu nyingi.
Kama hiyo haitoshi, ili kuthibitisha
kuwa mke wa mtu ni sumu, Baba Asha alimchoma jamaa huyo bisibisi kwenye
makalio hadi askari alipoingilia kati na kumchukua mtuhumiwa kisha
akamtoa nje.
Wakiwa nje ya gesti hiyo, Baba Tony
aliomba kujisafisha damu na baada ya hapo alipigwa pingu tayari kwa
kupelekwa Kituo cha Polisi, Pangani, Ilala...
No comments:
Post a Comment