Thursday, 6 March 2014

MCHUNGAJI ADAIWA KUISHI NA MKE WA MTU KINYEMELA ...NDUGU WATIMBA KANISANI...... MKE ACHOMOKA MBIO

MAKUBWA! Mchungaji wa Kanisa la Life in Christ Church Ministry maarufu kwa jina la Kwajoe lililopo Tabata-Segerea, Dar, Prophet Joseph au Nabii Joseph ameitwa polisi kisa kikidaiwa ni kuishi kinyemela na mke wa mtu aliyetajwa kwa jina la Martha Raymond (32).



Ndugu wa Martha wakiingia kanisani.
Kwa mujibu wa chanzo makini, kabla ya ishu hiyo kufika katika Kituo cha Polisi Tabata, Dar, mke huyo wa jamaa aitwaye Edward Kigoni ambaye pia ni mama wa watoto watatu, aliondoka kwa mumewe tangu Agosti mwaka jana hivyo katika kutafutwa ndipo ikabainika yupo kwa mchungaji huyo.

Ilidaiwa kuwa baada ya kugundua hivyo, mara kadhaa ndugu wa Martha wamekuwa wakifanya vikao kuhusu mgogoro kati ya wanandoa hao lakini Martha amekuwa mgumu kurejea nyumbani kwake.

Ndugu hao walidai kuwa kabla ya kugundua kuwa yupo kwa Nabii Joseph walikuwa wakimtafuta kwa njia ya simu na kumtaka arudi nyumbani lakini alitoa visingizio vya kuwa ‘bize’ na maombi, jambo lililosababisha kujitenga na masuala ya kifamilia.

Mke wa mtu Martha.
Akizungumza na paparazi, Machi 2, mwaka huu, baba mzazi wa Martha, Mao Raymond alidai hata yeye hajamtia machoni kwa zaidi ya miezi sita na mbaya zaidi hakuhudhuria hata msiba wa dada yake uliotokea Desemba, mwaka jana pamoja na kwamba alipewa taarifa kwa simu.

“Wakati tunamtafuta tuliambiwa anaishi kwa mchungaji huyo,” alisema baba huyo kwa masikitiko.

Machi 2, mwaka huu ndugu hao waliungana na kwenda kumchukua Martha kutoka katika kanisa hilo. 


Hata hivyo, hawakufanikiwa kutokana na Martha kugeuka mbogo akikataa katakata na kurudi nyumbani huku akitoka mbio kukimbilia kanisani.


Kwa kuheshimu kanisa, siku hiyo ndugu hao waliamua kumuacha kishingo upande na kwenda kutoa taarifa Kituo cha Polisi cha Tabata, Dawati la Jinsia ambapo mchungaji huyo alipelekewa barua ya wito ikimtaka ahudhurie kikao kituoni hapo kuhusiana na sakata hilo la Martha lakini si yeye wala Martha aliyehudhuria.

Paparazi walifuatilia sakata hilo hadi kanisani kwa Nabii Joseph ambaye baada ya kuelezwa madai ya ndugu wa Martha, alikanusha taarifa za kuishi na Martha.

Alipoulizwa kama anamfahamu Martha, alikiri kuwa anamfahamu kama mke wa mtu na muumini wake anayefanya shughuli zake kama kawaida.


Nabii huyo alipoulizwa kama alipata barua ya wito kutoka polisi, alikiri kupokea na kusema kuwa mara baada ya kupata wito huo, alimuita Martha na kumshauri aende kituoni kukutana na mkuu wa kituo ili amuelezee kila kitu.

Barua ya wito kutoka polisi kwa Prophet Joseph.
Alidai kuwa Martha alifanya kama alivyomshauri hivyo hakukuwa na sababu ya yeye kwenda kituoni kwa shauri hilo, taarifa ambazo zilikanushwa kituoni kwamba hawakufika wote.

Kwa mujibu wa mume wa Martha, Kigoni yeye anachotaka ni mkewe kurudi nyumbani huku akidai  kuwa kwa upande wake unatimia mwaka sasa hajaonana na mkewe zaidi ya kusikia kuwa yupo kwa Nabii Joseph.

 
Mke wa mtu.
“Ameondoka na kuniachia watoto watatu. Nashukuru tu kwamba kwa sasa wapo shule za bweni ila wakirudi likizo huwa napata shida sana kila siku wanamuulizia mama yao na mara nyingine wanamfuata hadi huko kanisani kwake,” alisema Edward.

No comments:

Post a Comment