Saturday, 27 April 2013

Bongo, mbwa kala mbwa..............

Huyu jamaa akaanza mbwembwe mapema kabisa, kwanza alichomoa simu: “Halo, nakwambia nimeshampata mpangaji kwa hiyo njoo uchukue hela yako…” nikaona we twende tu, mimi mwenyewe ni mtoto wa mjini. Akaendeleza swaga zake: “Elfu mbili yangu ipo?” Nikamuuliza ya nini? “Ala! Si nauli yangu? Mi nimeacha kazi kwa ajili yako hivyo…”


Kama u mfugaji wa ‘kitimoto’ basi ahirisha safari za wikiendi ili uwe na uhakika juu ya milo yao. Kama watapata ujauzito (samahani ni mimba) na kujifungua (sorry, kuzaa), hakika usipowapa msosi watakula watoto wao. Wakishamaliza watoto hao nao watafariki (sorry tena, watakufa). Hiyo ndiyo, mbwa kala mbwa.

Ukitaka kuisoma vyema falsafa hii ishi bongo. Dunia inakiri kuwa hii ni nchi ya kipekee kabisa. Bibi na mjukuu wake wanafanya uchangudoa Kinondoni wakati kijana na babu yake wanatapeli Sinza. Mjomba dalali anasakwa na wapangaji wakati Shangazi aliye kijumbe kwenye Vicoba hajulikani alipo.

Binafsi nilipigwa changa na dalali. Nilikuwa na nia ya kupanga chumba cha ofisi uswahilini, mwenye nyumba akaniambia haruhusiwi kufanya mkataba. Kama nataka kupanga nimtafute dalali. Kwanza nilishangaa, kwani dalali ndiye asiyeruhusiwa kufanya hivyo bila ya mwenye nyumba. Nikasema OK, mlete dalali, akaletwa.
Huyu jamaa akaanza mbwembwe mapema kabisa, kwanza alichomoa simu: “Halo, nakwambia nimeshampata mpangaji kwa hiyo njoo uchukue hela yako…” nikaona we twende tu, mimi mwenyewe ni mtoto wa mjini. Akaendeleza swaga zake: “Elfu mbili yangu ipo?” Nikamuuliza ya nini? “Ala! Si nauli yangu? Mi nimeacha kazi kwa ajili yako hivyo…”

Nikamjibu kuwa ndiyo kwanza nasikia kuwa unalipa kabla ya kuona bidhaa. Yaani unakwenda kuulizia pakiti ya Grants, unaanza kumlipa muuzaji kwa kazi ya kukuonyesha. Kama hana atakurudishia pesa? Pia nikamweleza kuwa siyo yeye niliyemhitaji. Shida yangu ni kufanya mkataba na mwenye nyumba.

Akaja juu: “We unaonekana mkorofi sana. Unauona mtaa huu na ule? Yote yangu. Upande ule wote ni wa Ahmada Mlevi na Sefu Mataputapu na ule kule ni wa Juma Mitungi. Kama huamini nenda kama utapata chumba. Ukisikia Mudi Chapombe ndiyo mimi.”

Nikaona Mtumeee! Nimeingia “choo cha walevi”. Hata hivyo, nikasema twende. Nikashangaa huyu jamaa alivyochukua uelekeo mwingine kabisa. Nikamkumbusha Chapombe kuwa nyumba nilishaiona, ilitakiwa idhini yake tu ili mkataba usainiwe. Lakini alikuja juu kama moto na kutishia kutoza faini ya “Mwanangu umemuonea wapi”. Tukaenda hadi kwenye uwanja wa wazi wa Manispaa. Kilikuwa kipindi cha mvua na pale uwanjani palijaa maji pomoni.
“Unaiona nyumba ile?” Alinionyesha katikati ya dimbwi. Palikuwa na kibanda mfano wa choo cha uswazi. “Safi kabisa kwa kufanya ofisi maana hamna majirani wa kukusumbua. Elfu Kumi na Tano tu, malipo ni miezi mitatu chumba na miezi miwili ya “king’amuzi (udalali).” Alikuwa siriaz, mishipa ya kichwa na mikono imemsimama kwa kubofya simu.

Nilimsogelea usoni kuona kama alimaanisha alichokinena au la, lakini hakuwa na lingine zaidi ya kukodolea dirisha la simu. Kwa jinsi nilivyomwelewa, alitaka nimpatie Shilingi Elfu Sabini na Tano; Arobaini na Tano za kodi ya nyumba na Thelathini za kwake. Niligundua baadaye kuwa Thelathini hizo hazihesabiki kwenye kodi, bali ndiyo ujira wa kazi yake.

Nilipandwa na ghadhabu kwa kuharibiwa muda, nikataka kuondoka bila kulipa ile Elfu Mbili ya nauli. Lakini jamaa aliniganda kama luba katika njia nzima. Niligundua kuwa tuliopishana nao walinichukulia kama niliyemdhulumu, kwani jamaa alijua kuongea. Nikajirudi kwa sharti la kupelekwa kwenye nyumba ile ya kwanza, tena kwa nauli ileile.

Shingo upande akanipeleka. Tulipoukaribia uchochoro wa kuingia hapo mjengoni tukakutana na jamaa mwenye ndevu za makusudi, yuko bwiiiii mpaka basi. “Enheee… Nimekubamba sijakubamba?” Aliunguruma. Jamaa yangu akaanza kujing’ata: “Mjomba nilikuwa nakupigia lakini mtandao…”

“Unipigie mie Polisi?” Mlevi alifoka. “Wewe si umeniacha kwa Mama Ngwendu nakunywa bapa sasa hivi tu? Haya lete Elfu mbili yangu.” Jamaa yangu naye akacharuka: “Aaaah! Hii ilikuwa kazi yangu sema mteja mwenyewe haelewi. Nimempeleka kule Hollywood kakataa ndo namleta kwako; kama vipi atakugea buku mbili zingine...

No comments:

Post a Comment