Saturday, 27 April 2013

HIVI NDIVO VYAKULA VINAVYOTUMALIZA..........................


Vyakula tunavyotakiwa kuvila, hatuvili tena na pengine upatikanaji wake ni wa shida, hivyo tunalazimika kula vilivyopo licha ya kuwa vina madhara kwa afya zetu. Hali hii imeongeza idadi ya wagonjwa na magonjwa sugu. Chakula kikuu cha mijini ni chips, kuku, mayai, soda, juisi za makopo au paketi, nyama choma na pombe. Pia kuna mkate mweupe, maandazi na chapati. Vyakula hivi huliwa kila siku, lakini ukivichambua utagundua havina faida yoyote mwilini zaidi ya kuingia na kutengeneza maradhi.


CHIPS Chips ambayo kwa kawaida hutengenezwa kutokana na viazi mviringo na kukaangwa kwenye mafuta, ni chakula kinachotakiwa kuliwa kwa kiasi kidogo na kwa nadra sana, kwa sababu kiko kwenye kundi la vyakula vyenye mafuta mengi ambavyo huliwa kwa uchache sana.Lakini hali halisi ni kinyume chake. KUKU Kwa kawaida, kuku wengi wanaotumika kwenye biashara ni kuku wa kizungu. Nyama ya kuku hawa haina virutubisho sawa na kuku wa kienyeji. Hii inatokana na ukweli kwamba kuku wa kizungu hulishwa madawa mbalimbali ya kuwakinga na magonjwa na hulishwa vyakula vilivyochanganywa madawa ili wakue upesi. Kwa mazingira hayo, nyama itokanayo na kuku wa aina hii haiwezi kuwa bora. Kiasili kuku huishi mazingira huru kwa kula vyakula ambavyo hujenga na kuukinga mwili wake dhidi ya magonjwa mbalimbali, kuku wa aina hii ndiye anayefaa kuliwa na kuleta faida ya nyama ya kuku inayokusudiwa. MAYAI Halikadhalika, mayai yanayopatikana kwa wingi mijini ni yale yatokanayo na kuku wa kufuga. Kiasili, mayai ya kuku wa kufuga, hayawezi kuwa sawa na mayai yatokanayo na kuku wa kienyeji. Huhitaji kuwa mwanasayansi kuona tofauti kati ya yai la kuku wa kienyeji na kuku wa kufuga, kwani mayai hayo yakipikwa huwa tofauti kwa ladha na hata rangi. Ni ukweli ulio wazi kuwa kuku wa kufugwa hulishwa vyakula vya kutengeneza ambavyo ndani yake huwekwa kemikali na madawa mbalimbali, wakati kuku wa kienyeji hula vyakula asili kwa kujitafutia wenyewe na mazingira wanayoishi ndiyo yanayowafanya wawe tofauti na bora. Hivyo ni dhahiri kwamba mayai tunayokula ya kuku wa kizungu yana madhara zaidi kuliko faida mwilini. SODA Moja ya vinywaji vinavyopendwa na kutumiwa na watu wengi ni pamoja na soda. Matangazo mengi ya biashara yanafanyika kutangaza kinywaji cha soda na kuonesha kuwa ni kinywaji ambacho hakina madhara kabisa kwa mtumiaji. Kwa matangazo hayo na kampeni hizo, familia nyingi zimeamini kuwa soda ni kinywaji bora na hata watoto wetu wamerithishwa imani hii. Lakini kwa upande wa pili wa kinywaji hiki, siyo kinywaji salama kama ambavyo imekuwa ikielezwa. Siwezi kusema moja kwa moja kuwa mtu huruhusiwi kabisa kunywa soda kama vile ni sumu, lakini watu walitakiwa kuelimishwa na kuelezwa madhara ya kupenda kunywa soda na athari anazoweza kuzipata mtu kiafya. Naamini tahadhari inayotolewa kwa wanywa pombe, hata kwa wanywa soda ilipaswa kutolewa pia. Utafiti unaonesha kuwa soda, pamoja na vikorombwezo vingine, huwekwa sukari nyingi kiasi kisichopungua vijiko sita katika chupa moja. Kiwango hicho cha sukari ni kingi zaidi ya mara tano ya kile 
kinachoruhusiwa kwa mtu kutumia kwa siku. Na madhara ya sukari mwilini ni mengi, yakiwemo ya kudhoofisha kinga ya mwili na viungo kwenye sehemu za maungio na pia huongeza uzito wa mwili. Ukitaka kujua soda ina madhara kiafya, fanya utafiti binafsi na utagundua haya ninayoyaandika. Kunywa soda zisizopungua tatu kwa muda mfupi, kisha lala usiku kama kawaida halafu wakati wa kuamka asubuhi, usikilize mwili wako.Utaamka ukiwa na maumivu mwili mzima, utajihisi uchovu, hasa sehemu za maungio, mfano wa mtu aliyefanya mazoezi mazito au kazi nzito siku iliyopita. Hiyo ni kutokana na kuingiza kiwango kingi cha sukari mwilini.



JUISI Katika hali ya kawaida, juisi ni kinywaji baridi kisicho na kilevi wala madhara kwa mnywaji. Lakini utakuwa sahihi ukizungumzia juisi zilizotengenezwa kwa matunda halisi bila kuongezewa vitu vingine. Katika zama hizi, hali iko tofauti, juisi nyingi tunazodhani ni vinywaji baridi visivyo na madhara kwa afya zetu na za watoto wetu, hali haiko hivyo. Juisi nyingi zinazouzwa kila sehemu ni feki. Ni jambo lakusikitisha kuona jinsi binadamu anavyojaribu kushindana na Mungu kwa kutengeneza vitu vinavyofanana na vile alivyoumba Mwenyezi Mungu kwa ajili yetu. Juisi nyingi hutengenezwa kwa kuchanganya maji, sukari na rangi zilizotengenezwa kwa kemikali mbalimbali zikiwemo zenye ladha ya matunda. Juisi za aina hii ndiyo nyingi na zinapatikana kila kona ya nchi hii, waathirika zaidi wakiwa watoto wetu ambao hupenda kunywa kwa kufuata utamu wa sukari nyingi zilizowekwa na ladha za matunda. Utafiti umeonesha kemikali (Additives) zinazowekwa kwenye vinywaji hivi, hudhoofisha kinga ya mwili na huwa chanzo cha magonjwa ya saratani na mengine hatarishi. Nakusihi kuacha kunywa kabisa juisi hizo na usimpe mwanao, unamuua. Ukiacha hizo juisi zinazotengenezwa kwa kutumia kemikali ‘mwanzo mwisho’, kuna juisi zingine zinazodaiwa kutengezwa kutokana na matunda, zipo za ‘machungwa’, nanasi’, ‘pasheni’, n.k. Yapo makampuni pia yanayojitapa kutengeneza juisi zao asilimia 100 kutokana na matunda na kwamba hakuna kinachoongezwa kingine. (100% fruit, No sugar added au No additives, huandika hivyo kwenye maboksi yao au makopo wanayoweka juisi. Hata hivyo, utafiti wa hivi karibuni umeonesha kuwa makampuni mengi yanadanganya walaji. Kwa sababu siyo kweli kwamba hawaongezi kitu kingine katika utengenezaji wa juisi zao za matunda. Imejulikana kuwa huweka vitu vya kufanya juisi ya kwenye boksi au chupa ikae kwa muda mrefu bila kuharibika, halikadhalika huweka vitu vya kuifanya juisi hiyo kuwa na ladha moja. Acha nikupe mfano. Katika hali ya kawaida, ukichuma machungwa matano ya mti mmoja, lazima yatakuwa na ladha tofauti, yote hayawezi kuwa na ladha sawa japo yote yanatoka mti mmoja. Kwa maana hiyo, kama ukitengeneza juisi kwa kutumia machungwa yaliyochumwa kutoka miti tofauti, ladha ya juisi lazima itatofautina. Lakini utashangaa kuona ladha ya jusi za maboksi zote zinafanana. Wanachofanya ni kuweka ladha moja kwenye utengenezaji wa juisi zao kabla ya kupeleka kwa mlaji. Halikadhalika, juisi ukishaitengeneza, haiwezi kukaa kwa muda mrefu bila kuharibika. Kwa hiyo, ili kuifanya juisi hiyo iweze kukaa kwa muda mrefu bila kuharibika, lazima iwekewe kemikali ya kuihifadhi na kuongeza vitu hivyo, hata kama Kwa maelezo hayo, hatushauriwi sana kunywa juisi hizo ‘ready made’ kwa sababu zimekosa uhalisia, kwani zina madhara kwa afya zetu, licha ya maelezo na matangazo mazuri tunayopewa na watengenezaji. Badala yake tutengeneza juisi majumbani mwetu wenyewe kwa kutumia matunda halisi ili kupata faida katika miili yetu. Jiepushe na matumizi ya sukari nyingi katika juisi unayoitengeneza mwenyewe, kwani kwa kufanya hivyo utakuwa unaiharibu, weka sukari kidogo sana ikiwezekana acha kabisa.  

No comments:

Post a Comment