Tuesday, 14 May 2013

Jamii ya wahaya nchini Tanzania

Inasemekana kuwa wahaya walitokea Misri na kupitia Uganda na hatimaye kuanza maisha katika eneo la Kagera kaskazini magharibi mwa Tanzania. 
Lugha ya watu wa kabila hili inafanana sana na ile ya jamii ya wanyankole wa nchi jirani ya Uganda. Tanaduni zao na hata mazao wanayolima (ndizi) vinafanana sana.
Kutoka Mwanza tulipanda meli kupitia Ziwa Victoria hadi Bukoba wanakoishi wahaya kwa wingi. Inachukua muda wa saa 16 kwa meli kutoka mwanza hadi Bukoba.
Tulipofika tulielekea kwenye makao ya mtemi wa wahaya ili kufahamu utamaduni na mila za jamii hii.
Tulikutana na mzee Petro Reueziani Butanga ambaye ni mshauri wa mtemi.
Kwanza alituonyesha alipokuwa akiishi mtemi aliyefariki Emmanuel Rukamba.
Zamani hakukuwa na kiberiti kwa hivyo jamii hii ilitumia vipande viwili vya mti uitwao Mrinzi.
Vipande hivyo vilivyokauka vikipekechwa hadi moto unapowaka.
Wakati wamishenari wa Ulaya walipowasili, eneo hilo lilikuwa maarufu kwa kuwa na Kadinali wa kwanza wa kikatoliki marehemu Laurian Rugambwa.
Aidha watu wa Jamii hii walizingatia sana elimu ikilinganishwa na makabila mengine nchini humo.
Mwaka wa 1978 eneo la Kagera lilivamiwa na jeshi la Uganda wakati huo chini ya uongozi wa Rais Idi Amin Dada lakini jeshi hilo lilishindwa kwa jeshi la Tanzania.
Kufikia mwaka wa 2006 idadi ya jamii ya wahaya ilikuwa zaidi ya watu milioni moja laki tatu.
Kabla ya kuwa na serikali ya taifa watemi ndio walitambuliwa kama wakuu wa jamii ya Wahaya.
Ndoa ni swala linaloheshimiwa katika kila jamii, na ni jambo linaloenziwa sana na jamii ya Wahaya.
Mahari ya Ng'ombe ama mbuzi ilitolewa kwa baba wa msichana kulingana na makubaliano ya pande zote mbili.
Mzee Petro Reueziani Butanga anaelezea.
Wahaya wana koo 8 ambazo ni Bumbira, Edangabo, Ganda-Kiaka, Hamba, Hangiro, Mwani, Nyakisisa, Ekiziba na Yoza.
Katika jamii ya wahaya kuna mambo ambayo ni mwiko kuyafanya yaani yamekatazwa kwa mfano kukata mti aina ya Mjuju na Mjunangoma.
Mti huo wa Mjunangoma uliheshimiwa sana kwani hapo ndipo mteni alipofanya tabiko, kwa hivyo unachukuliwa kama mti mtakatifu.
Aidha wanawake hawaruhusiwi kula wadudu aina ya senene ambao ni maarufu sana kwenye jamii hii, Mzee Butanga anaeleza
Iwapo mtemi angehitaji kutembea kwenda kijijini sokoni ama popote pale kwenye eneo lake basi alibebwa juu na watu wake akiwa ameketi juu ya machela maalum.
Watu walilibeba machela hiyo kwa zamu kutoka eneo moja hadi lingine. Na walifurahia sana kumbeba mtemi walichukulia fursa hiyo kama ni baraka.
Mtemi Emanuel aliyeafiriki alarithiwa na mwanawe wa kiume wa kwanza Innocent Rukamba.
Tulipofika kwenye makao ya mtemi alikuwa amesafiri kwenda mjini Dar Es Salaam.
Tulizungumza na mmoja wa kaka zake Bw. Mamwanzi Rukamba ambaye alitufamisha kuwa marehemu babake alikuwa na wake watano na watoto thelathini na watano.
Nyumba ya jadi ya Wahaya ilijengwa kwa miti na kuezekwa kwa nyasi kwenye paa na hata kuta zake.
Yaani hii ni nyumba ya nyasi kwa jumla hakuna udongo.
Sakafuni kumetandazwa nyasi maalum inayotumika kama zulia.
Tulipofika kwenye kijiji cha Kitwe tulikutana na Bibi. Bernedetta Dominic ambaye anaishi kwenye nyumba ya jadi ya Kihaya.
Kwenye nyumba hii moja wanaishi watu saba pamoja na mbuzi wao.
Bibi. Bernedetta ana umri wa miaka sabini ana ameshi kwenye nyumba hii kwa miaka 35. Anasema,
Utamaduni wa Wahaya una historia ndefu
Inaaminika kwamba wao ni kati ya watu wa kwanza kuanzisha shughuli za utengenezaji wa bidhaa za chuma cha pua.
Hatimaye tulisafiri hadi jumba la makumbusho la Kagera mjini Bukoba.
Hili ni jumba maridadi la makumbusho ambako kuna baadhi ya vitu vilivyotumiwa na jamii ya Wahaya kama vile vibuyu vya kuhifadhia pombe ya kienyeji.
Aidha kuna kifaa kilichotumiwa kuchemsha mawe ya Chuma aina ya iron.
Ukutani kuna picha za wanyama miti, ndege, samaki na nyoka wanaopatikana kwenye eneo la jamii ya Wahaya.
Mzee Leodegerius Rwekizo ni mwongoza wa watalii kwenye jumba hili la makumbusho, anatueleza kuhusu vitu vingi wanavyovihifadhiwa hapa.
Tulipoondoka Bukoba na kurejea Mwanza, tulikuwa na ufahamu mwingi kuhusu jamii ya Wahaya, inayolinda utamaduni wake hadi leo, inayoenzi vyakula vya jadi na kuzingatia maadili mema 

UTAMADUNI WA WAHAYA KULA SENENE.
    



 
Senene (Ensenene, kwa Kihaya) ni miongoni mwa wadudu wanaotumiwa sana na kabila la Wahaya mkoani Kagera kama kitoweo, pengine kuliko kabila lolote tangu enzi za mababu. 
Pamoja na wadudu hao kuheshimika katika kabila la Wahaya, historia kamili ya asili ya wadudu hao bado haijulikani. 

Mwanzoni senene waliliwa na wanaume peke yake. Wanawake walionywa wawe na haya siku zote na wasivunje mwiko kwa kula senene na vitu vyote vilivyokatazwa. Wanawake wote walikuwa na utii wakiheshimu mila na desturi za kabila lao hivyo kutokana na haya hiyo waliitwa “WAHAYA”.  

Wasichana walipeleka zawadi ya senene kwa wachumba wao kama ishara ya kuonyesha upendo na utayari wa kuolewa na mchumba huyo. Msichana ambaye hakufanya hivyo uwezekano wa...


No comments:

Post a Comment