Lucylight Mallya akizungumzia jinsi alivyojipanga katika masuala ya elimu.
Lucylight ambaye ni mtoto wa kwanza katika familia ya watoto wanne, alisema siri kubwa katika kufaulu kwake ni kufahamu nini anachokitaka katika maisha yake na kuyapenda masomo ya sayansi.
Ni kauli ya mwanafunzi yatima aliyeoongoza kwa ufaulu kidato cha sita
Dar es Salaam. Wakati matokeo
mengine ya Mtihani wa Taifa wa Kidato cha Nne mwaka jana yakitoka na
ufaulu kuongezeka, matokeo ya kidato cha sita nayo yametangazwa rasmi
huku msichana yatima, akiongoza kitaifa katika kufaulu masomo ya
sayansi.
Msichana huyo, Lucylight Mallya (20) alikuwa ni mwanafunzi wa Shule ya Wasichana ya Marian, iliyoko mkoani Pwani.
“Kukosa wazazi kulinifanya nisome kwa bidii zaidi
kwa kuwa nilijua kuwa nina majukumu makubwa, maana nina wadogo zangu
watatu,” alisema Lucylight. Baba yake alifariki mwaka 2005 na mwaka
uliofuata akafariki mama yake.
Lucylight ambaye ni mtoto wa kwanza katika familia
ya watoto wanne, alisema siri kubwa katika kufaulu kwake ni kufahamu
nini anachokitaka katika maisha yake na kuyapenda masomo ya sayansi.
“Sikuwa nikisoma ili nifaulu mitihani, nilikuwa
nasoma ili kuelewa kwa kuwa nilifahamu nataka kuwa nani baadaye katika
maisha yangu,” alisema Lucylight.
Msichana huyo ambaye pia aliongoza katika matokeo
ya kidato cha nne mwaka 2010, alisema sababu nyingine ya yeye kuwa
kinara wa masomo ya sayansi nchini, ni kuandaliwa vyema na walimu wake
na kuiheshimu ratiba yake ya kila siku.
Alisema siku zote aliifuata ratiba ya kujisomea na alipenda zaidi masomo kwa njia ya vitendo kuliko nadharia.
“Unaposoma kwa njia ya vitendo, unalifahamu somo
zaidi kuliko kwa njia ya nadharia. Ingekuwa shule zote zinafundisha kwa
vitendo, wanafunzi wengi wangebaini vipaji vyao mapema,” alisema
Lucylight.
Mwanafunzi huyo mwenye ndoto ya kuwa daktari,
alilieleza Mwananchi kuwa, huko nyuma aliyapenda masomo ya biashara
lakini kwa kuwa alikuwa na uwezo pia katika masomo ya sayansi, walimu na
wazazi walimshauri ajikite zaidi katika sayansi.
Lucylight, amesoma Shule za Msingi Olimpio na St
Mary’s zote za jijini Dar es Salaam na Shule ya Sekondari ya Wasichana
ya Marian kuanzia kidato cha kwanza hadi cha sita.
Akizungumza na Waandishi wa habari, baba mlezi wa Lucylight,
Dominic Mallya ambaye ni baba mkubwa alisema mtoto huyo ana kipaji na
juhudi binafsi.
No comments:
Post a Comment