Thursday 19 September 2013

UEFA yaomba kusubiri

Wakuu wa soka barani Ulaya wameshindwa kuafikiana juu ya mjadala kuhusu kama fainali ya Kombe la Dunia ya mwaka 2022 iahirishwe kutoka majira ya joto hadi majira ya baridi nchini Qatar.

Platini
Michel Platini
Ingawa wanachama 54 wa UEFA hapo jana waliunga mkono mabadiliko yanayotishia kuvuriga ratiba ya msimu mzima wa soka barani Ulaya, chombo cha washauri wake wa sera kimekataa kukubali lolote kabla ya mashauriano ya kina na FIFA.
Wanachama 54 wa UEFA walisema jumatano kua hofu yao ni kuhusu hali ya mashabiki na wachezaji watakaokwenda huko wakati wa Joto la kupindukia nje ya viwanja.
Vilabu, kamati za Ligi na mashirika ya wachezaji yanayoshirikiana na vyama vya soka Kitaifa kuunda Baraza la mipango ya wachezaji wa kulipwa kwa pamoja wamekataa kumruhusu Rais wa UEFA idhini ya kuafiki mabadiliko, ambayo Rais wa FIFA Sepp Blatter anasema baraza lake litachukua uwamuzi mwezi ujao

Siyo makubaliano, alisema Theo van Seggelen, Katibu mkuu wa FIFPro, akizungumza na shirika la habari Associated Press.
Van Seggelen aliongezea kusema kua joto kali la majira ya joto nchini Qatar ndio mojapo ya masuala nyeti ambayo bado yanahitaji majibu.
Siku moja kabla ya sintofahamu hii ya Alhamisi, wanachama wa UEFA walimpa Rais wao Platini idhini ya kuidhinisha mpango wa FIFA wa kutaka mashindano yafanyike mwezi Januari nchini Qatar.
Platini anatakiwa kupima maoni tofauti ya wanachama wake atakapouongoza ujumbe wa watu nane kwenye mkutano wa wanachama 27 wa kamati kuu ya FIFA mjini Zurich kuanzia tareh 3 hadi 4 October.
Blatter, ambaye ni mwanachama wa Kamati ya Olimpiki Kimataifa amependekeza fainali ifanyike mwezi Novemba mwaka 2022 kuepuka athari ya aina yoyote juu ya michezo ya Olimpiki ya majira ya baridi yanayotazamiwa mnamo mwezi febuari

No comments:

Post a Comment