Monday, 13 January 2014

HARI YA KIMATAIFA:Waziri mkuu UAE akiri kutomtendea haki Mmarekani

DUBAI:
Waziri mkuu wa Umoja wa Falme za Kiarabu Sheikh Mohammed bin Rashid Al-Maktoum, amesema leo kuwa namna alivyotendewa raia wa Marekani aliekaa gerezani kwa miezi tisa kwa kosa la kuweka video ya kuchekesha kwenye mtandao wa Youtube haikuwa ya haki. Waziri mkuu huyo ameliambia shirika la utangazaji la Uingereza BBC katika mahojiano kuwa hilo lilikuwa kosa ambalo taifa lake limejifunza .. 

Raia huyo wa Marekani Shezanne Cassim aliwekwa kizuwizini mwezi Aprili na kuhukumiwa kifungo cha mwaka moja mwezi Desemba  kutokana na video yake hiyo, ambayo inawadhihaki vijana wadogo wa falme hiyo wanaoiga utamaduni wa muziki wa kizazi kipya cha Marekani. Cassim ambaye alitozwa faini ya dola za Marekani 2,700 aliachiwa wiki iliyopita, na kurudi Marekani akisema hakufanya kosa lolote.

No comments:

Post a Comment