Kampuni ya kutengeneza magari ya Ujerumani
BMW, imesema leo kuwa iliuza magari mengi
mwaka 2013,kuliko ilivyowahi kufanya hapo kabla
na inalenga kuzidisha idadi hiyo mwaka huu.
BMW ilisema katika taarifa kuwa iliuza jumla ya
magari milioni 1.964 mwaka uliyopita, hii ikiwa ni
ongezeko la asilimia 6.4 kutoka rekodi ya mwaka
uliyotangulia wa 2012.
Kundi hilo linamiliki aina tatu za magari- BMW, Mini
na Rolls-Royce, na linatengeneza pikipiki pia. Mauzo
ya BMW pekee duniani yaliongezeka kwa asilimia
7.5 hadi kufikia milioni 1.655.
Mauzo ya magari ya Mini yalikuwa 305,030 duniani
kote wakati mauzo ya Rolls-Royce yaliongezeka kwa
asilimia 1.5 na kufikia 3,630.
No comments:
Post a Comment