Bila shaka umeshawahi kusikia minong’ono kuwa wanaume warefu wana
mvuto mkubwa kwa wanawake tofauti na wenzao wafupi. Bila shaka umewahi
kuisikia hii kwa baadhi ya wanaume wakikiri kuwa wanaume warefu
wanakubalika kirahisi kwa wanawake.
Nimelazimika kufanya utafiti wa kisomi ili kuona kama kuna ukweli
wowote au ni maneno tu ya mitaani; aidha nikajaribu upande wa pili kwa
maana ya kuzungumza na wanawake ili nisikie wenyewe wanachosema, wengi
wamekiri kuwa wanaume warefu wana mvuto sana.
Baadhi yao wanadiriki hata kusema kwamba huwa wanatamani kuwatongoza,
shida ni mila na desturi za kwetu haziruhusu mwanamke kumtongoza
mwanamume, mwingine akaniambia kuwa wanaume warefu wengi wao wanajiamini
zaidi kuliko wafupi.
Pia watu warefu wanajikubali sana, wapo wengi tu wanaokubali kuwa
wanaume warefu wanakuwa ni wenye mvuto…je, wewe una maoni gani?
Mtafiti mkongwe katika masuala ya mapenzi duniani, Fisher, Helen
katika kitabu chake alichokipa jina Why We Love yaani kwa nini
tunapenda, kilichochapishwa Marekani (ISBN 0-8050-6913-5), anasema kuna
ukweli juu ya jambo hili.
Anasema imani ya wanawake wengi ni kwamba wanaume warefu wana
mwonekano mzuri. Pia kina dada wanajiona wako salama zaidi
wanapoongozana na mtu mrefu tofauti wakiongozana na mtu mfupi.
Ingawa wengine wanahusisha urefu wa mwanaume na urefu na
viungo…lakini kuwa na fimbo kubwa na mwingine kuwa na fimbo ndogo, haina
maana kwamba mwenye fimbo kubwa atampiga mwanafunzi akaumiza zaidi
kuliko mwenye ndogo…hapa ni suala la ujuzi.
Kufikiri kwamba wanaume warefu ni bora kwa sababu ya urefu wao,
huenda ni imani isiyo sahihi sana, ingawa kwa kiasi ina ukweli hasa
katika kimo cha mtu…mara nyingi urefu wa vidole vya mwanaume vinaweza
kukupa mwelekeo wa urefu wa kwingine.
Msomi Simpson, John, ed. (1989 toleo la pili), kitabu maalumu kuhusu
umbo la mwanaume, kilichochapishwa na Chuo Kikuu cha Oxford University
anasema kwa kiasi fulani huwezi ukawa na vidole vifupi, halafu
ukatudanganya kuwa kwingine kutakuwa kurefu, ni ngumu!
Aidha Ponchietti R, Mondaini N, BonafË M, Di Loro F, Biscioni S,
Masieri L (2001) katika kitabu chao kiitwacho “Penile length and
circumference’ kinachozungumzia maumbile ya wanaume na utahiri,
kilichochapishwa Italia, wanasema udogo au ukubwa wa chochote hauna maana kama ndio kitakuwa kizuri au kibaya; kuwa na sura mbaya haina maana una roho mbaya wala kuwa na sura nzuri haina maana una tabia nzuri.
Wanawake walio wengi huvutiwa na wanaume walio warefu…achilia mbali
baadhi ya wanawake kupenda kwa sababu ya fedha, kisaikolojia wanajisikia
fahari kuwa na mwanaume mrefu.kilichochapishwa Italia, wanasema udogo au ukubwa wa chochote hauna maana kama ndio kitakuwa kizuri au kibaya; kuwa na sura mbaya haina maana una roho mbaya wala kuwa na sura nzuri haina maana una tabia nzuri.
Msomi mwingine mkongwe katika masuala ya mapenzi, Kierkegaard, S¯ren (2009) anasema katika utafiti wake alioupa jina Works of Love, huko New York City, kuwa ni kutokana na sababu za kisaikolojia zaidi kufikiri kuwa wanapokuwa na wanaume warefu wanakuwa salama zaidi, hata hivyo anasisitiza kuwa wakati mwingine tabia za mtu hazitokani na urefu au ufupi wake, bali huja kiasili.
Watafiti wengine Singer, Irving (1966) walisema katika kitabu chao cha The Nature of Love yaani asili ya mapenzi kilichochapishwa na Chuo Kikuu cha Chicago Press na kurudiwa upya mwaka 1984, kuwa wakati mwingine imani hiyo siyo sahihi.
No comments:
Post a Comment