DENTI wa Shule ya Sekondari ya Erkisongo (jina tunalo) iliyopo wilayani
Monduli mkoani Arusha, anadaiwa kumchoma kisu katika paji la uso baba
yake mzazi Daudi Msemo baada ya kuonywa kuachana na tabia ya kuchanganya
ngono na masomo.
Denti wa Shule ya Sekondari ya Erkisongo anayedaiwa kumchoma kisu katika paji la uso baba yake mzazi Daudi Msemo.
Hayo yamesemwa na Fatuma Daudi ambaye ni mama mzazi wa mwanafunzi
huyo mara baada kutokea tukio hilo la kusikitisha hivi karibuni nyumbani
kwao Monduli ambapo denti alipofikishwa polisi alisema alifanya kitendo
hicho kwa sababu baba yake alitaka kumbaka.
“Binti yetu huyu amekuwa
akibadilika tabia na mara nyingi tumekuwa tukimuonya aache vitendo vya
umalaya akiwa mwanafunzi lakini bado amekuwa akiendeleza tabia yake hiyo
ambayo sisi wazazi tumeona ni kudharau maagizo yetu,” alisema Fatuna
alipozungumza na gazeti hili.
Aliongeza kuwa, tabia hiyo ilikuwa ikimfanya mwanafunzi huyo kuchelewa kurudi nyumbani na wakati mwingine kutorudi kabisa.
Mama
huyo alisema, kutokana na tabia hiyo waliamua kumdhibiti ili aache
lakini matokeo yake alimchoma kisu baba yake na akamsingizia alitaka
kumbaka hali iliyowalazimisha polisi kuwaweka ndani wote.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas.
Fatuma alikwenda mbali zaidi kwa kuwaomba baadhi ya wanajeshi ambao
wana uhusiano wa kimapenzi na binti huyo waache kwa kuwa ni kinyume cha
maadili na mwanaye bado ni mwanafunzi wa kidato cha nne.
Maelezo ya
denti huyo yalimfanya baba mzazi kuahidi kujiua baada ya kutoka kituoni
hapo akidai amedhalilishwa sana, hali iliyowafanya polisi kuamua
kuendelea kumshikilia licha ya kwamba walishamruhusu kutoka baada ya
mkewe kumtetea.
Afisa mmoja wa jeshi la polisi ambaye hakutaka
kuandikwa jina lake gazetini kwa kuwa siyo msemaji alithibitisha kutokea
kwa tukio hilo.
“Tunaendelea na uchunguzi na wote wawili, baba na
mwanaye tunawashikilia ili kubaini chanzo cha kutokea kwa tukio hilo,
baada ya uchunguzi maelezo zaidi utapewa na kamanda wa mkoa afande
Liberatus Sabas, kwani ndiye msemaji wa jeshi mkoani hapa,” alisema
afisa huyo.
-GPL
No comments:
Post a Comment